Omary. Amebanwa maswali mengi na mwandishi wetu Hamida Hassan lakini
kutokana na jina la kolamu hii, tunakuletea maswali 10 ‘hot’ aliyoulizwa
na yeye kutoa ushirikiano katika kuyajibu licha ya kwamba aliachwa
kijasho chembamba kikimtoka.

Staa wa filamu za Kibongo Vanitha Omary.
Ijumaa:
Kuna hizi tetesi kwamba huyu mume wako wa sasa alikuwa ni mpenzi wa
rafiki yako Joan Matovolwa lakini wewe ukampora na mkaishia kuoana, hili
unalizungumziaje? Vanitha: (Kicheko) Ukweli ni kwamba mimi na Joan ni
marafiki wakubwa na hilo unaloongea halina ukweli wowote. Maneno hayo
yaliibuka baada ya kuwepo taarifa kuwa nataka kuolewa.
Ijumaa:
Wewe ni msanii lakini ni mke wa mtu, siku ukiwa hujaenda kwenye shughuli
zako za kisanii uwapo nyumbani huwa unafanya nini? Vanitha: Huwa
napenda kupikapika. Wewe ni mke wa mtu halafu ni sanii, je unapokuwa
nyumbani unapenda kumpikia chakula gani mumeo?
Vanitha: Nikiwa
nyumbani napenda kumpikia baby wangu chakula kizuri ambacho ni kipya.
Ijumaa: Je, pale unapokuwa faragha na mumeo unapenda kumtega kwa vivazi
gani?Vanitha: Ukweli huwa simtegi kwa mavazi, napenda kumtega kwa kukaa
mtupu kwani wakati huo huwa ni wake, kwa nini nimfichie mali zake?
Ijumaa: Ni upi ugonjwa wako uwapo faragha na huyo mumeo?
Vanitha: Napenda sana kumkumbatia na yeye anikumbatie. Kale kajoto
kanakotokea huku tukinong’onezana maneno matamu mimi nabaki
kusinziasinzia.
Ijumaa: Watu wanasema wanaume hawatabiriki kwa
kuchepuka, hivi siku ukimfumania mumeo utafanya nini?Vanitha: Naomba
Mungu isitokee kwani nahisi nitafanya tukio baya na kumuacha siwezi,
dah! Nahisi kutetemeka ukiniambia hivyo.
Vanitha Omary akipozi.
Ijumaa:
Mastaa wana skendo ya kuchukua waume za watu, wewe unamlindaje mumeo
asinaswe na wezi hao? Vanitha: Siwezi kusema nitamlinda kwani sijui mtu
anakuwa na nia gani na atakuwa amejipanga vipi ila nabaki kumuomba Mungu
amuepushe mume wangu na vishawishi.
Ijumaa: Kuna wanawake ambao
eti wanaona kuwapa waume zao mapenzi kinyume na maumbile ndiyo
kuwashika, wewe kwako likoje hili? Vanitha: Mungu aniepushie mbali kwani
ni jambo baya sana, sijawahi na sitowahi, nawaomba wanaofanya hivyo
kuacha kwani Mungu hapendi.
Ijumaa: Ni kitu gani kimewahi kukufurahisha katika maisha yako?
Vanitha: Nilifurahi sana siku niliyofunga ndoa na mume wangu kwani
tulipitia mikikimikiki mingi. Tumekaa kwenye uchumba kwa muda mrefu.
Ijumaa: Siku uliyohuzunika sana unaweza kuikumbuka?
Vanitha: Ni siku bibi yangu alipofariki, nakumbuka nilikuwa katika
wakati mgumu kwani yeye ndiye alikuwa mlezi wangu na nilikuwa na
ujauzito.
Ijumaa: Mbali na sanaa, ni kazi gani unaifanya?
Vanitha: Mimi ni mbunifu wa kupamba nyumba, nafanya kazi ya kuwadizainia
watu nyumba zao kwa mapambo mpaka muonekano mzima wa nyumba .
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33





