 |
Blandina Chagula ‘Johari’ |
STAA
wa filamu, Blandina Chagula ‘Johari’ ameamua kuvunja ukimya wa muda
mrefu baada ya kuweka wazi mwanaume ambaye anahitaji amuoe na sababu
inayomfanya asijichanganye na mastaa wenzake.
Katika makala haya Johari amefunguka mengi, msome;
Mwandishi: Kwa nini mara nyingi hupendi kujichanganya na mastaa wenzako?
Johari: Ujue
nina kampuni ambayo wakati wote nahitajika kuwepo hapo, na kama
kujumuika, najumuika na wenzangu pale pa muhimu kama kwenye misiba.
Mwandishi: Tangu
umeingia katika tasnia ya filamu kuna mastaa ambao mara nyingi
wanawaweka wazi wapenzi wao lakini wewe haijatokea ni kwa nini?
Johari: Unajua
kwa sasa ni kama dada wa mastaa, kitendo cha kuwaweka wazi wapenzi,
wengi wanakuwa akili zao hazijakomaa, lakini najitambua na ninaelewa
akili za wanaume, unamtambulisha leo kesho kakukimbia utakuwa
unatambulisha wangapi?
Mwandishi: Mbona kuna tetesi kuwa Ray alikuwa anakukataza kumtaja hovyo wakati wengi wanajua ndiye mpenzi wako?
 |
Ray na Johari Enzi za Mapenzi yao |
Johari: Sipendi kuzungumzia chochote kuhusu Ray kwa sababu kila mtu ana maisha yake na kwa nini anikataze?
Mwandishi: Kuna
wanaume wengi huko nje wanapenda kukuposa lakini wanaogopa wakijua kuwa
mastaa hawawezi kuposwa na watu wa kawaida, unalizungumziaje hilo?
Johari: Hapana!
Kwanza kwa upande wangu nahitaji kuolewa na mwanaume wa kawaida ambaye
anaweza kunijali na kujua thamani yangu na siyo wa kujibweteka, ajue
kuchakarika na wala sichagui, maelewano tu.
Mwandishi: Mastaa wengi hawafanyi kazi mara nyingi wanategemea filamu pekee ambazo haziwasaidii, unalizungumziaje hilo?
Johari: Hilo
hata mimi linaniumiza sana kwa kuwa mastaa wengi wa kike hawajitumi,
asilimia kubwa ni tegemezi kwa wanaume ila ninachoona ni bora kuridhika
na moja ya kwako kuliko elfu moja ya wenzako.
Mwandishi:
Mwandishi: Mara nyingi huonekani katika kumbi za starehe, kwa nini?
Johari: Kikubwa ni kazi na kukosa muda, pia sipendi kujichanganya sehemu kama hizo.
Mwandishi: Mna bifu lolote na Chuchu Hans?
Johari: Mmmh! Sina, sipendi zaidi kuzungumzia hilo, samahani.
Muda unazidi kusonga mbele na karibia mastaa wengi wana watoto, vipi wewe unangoja nini?
Johari: Sidhani kama kuna mtu ambaye hatamani kuwa na mtoto, kwa upande wangu lazima nitafute baba mwema nitakayemzalia.
Mwandishi: Haya asante Johari.
Johari: Karibu tena.