MAPENZI:WANAUME, TYPE HII YA MSICHANA USIBONYEZE ASEE, NI SHIDAAAH,CHEKI HAPA.

Admin Updates10 years ago6 Views

Hakikisha unawakwepa aina hii ya wanawake ili usijiingize kwenye matatizo. Nitakwambia ni kwa nini…..

1.Demu wako wa zamani
Ni vizuri kutorudia mahusiano ya zamani na zaidi kama kwenye mahusiano
yenu ya mwanzo mambo hayakuishia kwa uzuri. Sababu kuu ya msingi,
kiukweli ni kwamba hakika mwanzoni mlikuwa hamuendani na ndio sababu ya
iliyopelekea kuvunjika kwa mahusiano yenu, ndani ya hizo sababu kuna
vitu vilivyopolekea kutokea kwa hayo, ukichunguza na kuziangalia kwa
makini utagundua ni za asili na ambazo si rahisi kwa mmoja wenu
kuzibadilisha sababu ni vitu au mambo ambayo yatakuwa ni ya damuni.*

2.Dada wa rafiki yako kipenzi
Epukana na kujiingiza kwenye mahusiano na dada wa rafiki yako. Si tu
kwamba utaweza kujiingiza kwenye uhasama na chuki kama mambo
hayatakwenda sawa, ila pia utaweza kujiweka kwenye mazingira ya kujikuta
siku moja unapigwa hata ngumi za uso sababu tu ulimuumiza dada yake.
Pia, utaweza kumkosa mtu ambaye ndie alikuwa ni kimbilio lako kwa mambo
mbalimbali pale ambapo itatokea wewe na dada yake mambo kutokwenda sawa,
sababu hapo patakuwa na mgongano wa kimaslahi kwa huyo rafiki yako.*


3.Wanawake wenye mambo mengi*
Kiukweli, kutoka na watu kama
hawa kinaweza kuwa ni kitu cha kufurahisha, ila mwisho wa siku
itakuingiza kwenye matatizo. Mara zote kumbuka ni vyema kuwa salama
kuliko kujuta. Usijiingize kwenye majaribu ambayo utakuja kuyajutia kwa
maisha yako yote.*

4.Wanawake wanaopenda hela kupitiliza (Wachunaji)
Kuwa mbali nao, labda kama unataka salio lako limalizike pasipo wewe
kujifahamu. Naamini hili kila mmoja analifahamu na halihitaji darasa
zaidi.

5.Demu wa zamani wa rafiki yako
Kama unathamini
urafiki wako na mshikaji wako achana na habari ya kutoka na aliyekuwa
demu wake. Mambo yanaweza kubadilika na kuwa kama au zaidi ya
yaliyotokea kwa rafiki yako na ikaja kula kwako zaidi. Wakati mwengine
inaweza tengeneza chuki kati yako na rafiki yako, huku akiamini kwamba
ulikuwa unatoka au kumnyemelea demu wake toka zamani.

Wadau mademu wapo wengi sana, fanya kutafuta wengine nje ya hawa….. ni ushauri tu.

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.