KUTANGAZA NIA YA URAIS 2015 WASANII WAGAWANYIKA VIPANDE WENGINE KWA LOWASA NA WENGINE KWA MEMBE..WAONE HAPA

Admin Updates10 years ago5 Views

Waziri wa mambo ya nje Bernard Membe.

MPASUKO!
Zikiwa zimesalia takriban siku 31 kabla ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kumpitisha mgombea mmoja wa urais atakayechuana na vyama vya upinzani,
imebainika kuwa mastaa wa filamu na Bongo Fleva wamegawanyika vipande
huku wakiwa kwenye msuguano mkali kufanikisha ushindi wa makada Bernard
Membe na Edward Lowassa, Risasi Mchanganyiko linapa mchapo kamili.

WAJIPAMBANUA
Taarifa kutoka ndani
ya tasnia hizo ambazo zina nguvu ya ushawishi katika jamii zimeeleza
kuwa, Membe ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, kwa kiwango kikubwa amewakamata wasanii wengi wa Bongo Movies
wanaomuunga mkono huku Lowassa (Waziri Mkuu wa zamani) akiwa
amewadhibiti vilivyo mastaa wa Bongo Fleva.
“Ni mpasuko wa aina yake,
Membe ameonekana kuwakamata kisawasawa wasanii wa Bongo Movies na ndiyo
maana hata juzi (Jumapili iliyopita), mastaa wengi wa filamu walikwenda
Lindi kumuunga mkono alipokuwa anatangaza nia.
Membe akiwa na wasanii wa bongo movie.
WANACHOKIAMINI
“Mastaa
kama Steve Nyerere (Steven Mengere, JB (Jacob Steven), Ray (Vincent
Kigosi), Dude (Kulwa Kikumba, wanaoonekana katika picha ndogo ukurasa wa
kwanza) Hashim Kambi, Ester Kiama (Ester wa Dude) Swebe (Adam Melele)
na wengine kibao wameshatonywa kuwa CCM itampitisha Membe hivyo
wanamuunga mkono kwa nguvu zote kuhakikisha wanapata sapoti pindi
atakapopitishwa na chama chake kisha kuwa rais.
WENGINE HAWAJIPAMBANUI
“Timu
ya wasanii wa filamu wanaomuunga mkono Membe ni kubwa sana sema wengine
hawajajitokeza hadharani lakini wanapambana chini kwa chini kwani wana
uhakikia kwamba piga ua, CCM itampitisha tu.
Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa.
LOWASSA SASA
“Kwa
upande wa Lowassa, amepata zaidi mastaa wa muziki. Nao wameamua
kujipambanua kwa kuwa nao wametonywa kwamba rais ni Lowassa. Wanaamini
hivyo, wanapambana kweli kuhakikisha anachukua mikoba ili aje awatimizie
mahitaji yao.
“Utakumbuka wiki chache zilizopita alitangaza nia kule
Arusha wasanii kibao wa muziki wakiongozwa na Diamond (Nasibu Abdul),
Nay wa Mitego (Emmanuel Elibariki), Khadija Kopa na wengine wengi tu
walienda kumuunga mkono. Kuna nyimbo 21 maalum za Lowassa zilizotungwa
na wasanii mbalimbali na kusambazwa kama njugu kwa makundi tofauti ya
watu wakiwemo waendesha bodaboda.
WAPO WA CHINI KWA CHINI
“Kama
ilivyo kwa Membe, Lowassa naye ana timu kubwa sana katika Bongo Fleva
ambayo inapambana chini kwa chini. Kuna wasanii kama R.O.M.A (Ibrahim
Mussa), Juma Kassim (Nature), Recho (Winfrida Josephat) wote ni Team
Lowassa. Yaani uchaguzi wa mwaka huu ni full mpasuko,” zilieleza taarifa
hizo.
MBIVU MBICHI, JULAI 12
Kwa mujibu wa ratiba ya chama cha
mapinduzi CCM, mgombea wa urais atajulikana Julai 12, mwaka huu mara
baada ya kikao cha Mkutano Mkuu kumalizika.

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.