WEMA NA LINAH SASA WAKARIBIA KUCHAPANA NGUMI…CHEKI BALAA LAO

Admin Updates10 years ago7 Views

NI shiida! Siku chache baada ya msanii
wa muziki wa kizazi kipya nchini, Esterlina Sanga ‘Linah’ kulalamika juu
ya kitendo cha Wema Sepetu ‘Madame’ kumchukua aliyekuwa bwana’ake
Nangari Kombo, muigizaji huyo ameibuka na kutoa maneno yanayoashiria
kejeli, kuwa aache presha, kwani zile ni picha tu!

Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madame’.
Katika gazeti la Risasi Jumamosi, toleo
lililopita, iliripotiwa na kuchapishwa habari na picha zilizomuonyesha
Madame akiwa amepozi kitandani na kijana huyo, aliyepata umaarufu baada
ya kuingia ndani ya eneo la kuchezea katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar
es Salaam mwaka 2010, wakati wa mechi kati ya Brazil na Taifa Stars na
kumkumbatia kiungo nyota wa mabingwa hao wa zamani wa dunia, Kaka.
Lakini Risasi Mchanganyiko lilipotaka
kujua maoni yake juu ya shutuma hizo, Wema alisema kupiga picha na
Nangari hakumaanishi mapenzi, kwani yeye ni mtu wa watu na picha kama
hizo hupiga na marafiki zake wengi tu, hivyo Linah asiwe na shaka naye
hata kidogo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Esterlina Sanga ‘Linah’.

“Nilipiga naye kama ninavyoweza kupiga
na marafiki wengine kama akina Martin Kadinda, Petit Man na wengineo.
Sina uhusiano naye wa kimapenzi, naomba aamini kuwa ni rafiki tu wa
kawaida,” alisema Wema na kuibua maswali juu ya aina ya uswahiba wa
kawaida wa kupiga picha kitandani na mpenzi wa mtu!

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.