MWANASHERIA CHADEMA APELEKWA INDIA KWA MATIBABU..NI HUYU HAPA

10 years ago104 Views

Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mabere Marando, amepelekwa nchini India na familia yake kwa ajili ya kupata matibabu zaidi — yameripoti magazeti la MTANZANIA na MAJIRA siku ya Jumanne, Septemba 15, 2015.
Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano Msaidizi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), John Steven, alisema Marando aliondoka juzi na baadhi ya ndugu zake.
“Wameondoka Jumapili kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi, wenyewe walisisitiza tusitaje ugonjwa unaomsumbua ndugu yao, na kwamba ataeleza mwenyewe (Marando) pindi atakapopona”

Marando ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA, alifikishwa hospitalini hapo usiku wa Septemba 7, mwaka huu, baada ya kuugua ghafla akiwa nyumbani kwake na kuazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete karibu wiki nzima kwa ajili ya matibabu.

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.