MH.RIDHIWANI KIKWETE APAGAWA KWA NYIMBO MPYA YA BELL 9

9 years ago102 Views

Mbunge wa Chalinze na mdau mkubwa wa sanaa na michezo nchini Ridhiwani Kikwete ameshindwa kujizuia na kuweka wazi mahaba yake kwa ngoma mpya ya Belle 9 iliyozinduliwa mwishoni mwa wiki ya ‘GIVE IT TO ME’.
Ridhiwani ambaye alikuwa ni miongoni mwa wadau waliohudhuria uzinduzi huo alizungumza na eNewz ya EATV na kusema kuwa anapongeza sana Belle 9 kwa hatua hiyo video ni kali sana na yeye kama mbunge na kijana huwa anapenda kushirikiana na vijana wenzake ili kuweza kukuza sanaa yetu.
“Niliona kwenye page yake ya instagram akiwa Afrika ya Kusini kwa ajili ya ku’shoot’ video yake na kuwasiliana naye kuwa akirudi tuonane na kweli aliporudi tulikaa tukaongea akaniomba sehemu pale nyumbani afanyie huo uzinduzi nikampatia ndiyo kama unavyoona “

Pia aliongeza kwa kusema kwamba kitu kikubwa ambacho kimemvutia sana katika video hiyo ni jinsi alivyotembea na “beat” ya wimbo huo pamoja na ile sehemu jinsi anavyojitoa kwa mpenzi wake.
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.