ZIJUE HIZI SIFA TANO ZA MWANAUME ANAYEKUTAMANI

Admin Updates9 years ago8 Views


NI Jumanne tena! Naamini wasomaji wangu wote mpo sawasawa na tayari kupokea mada mpya ya wiki hii. Habari kubwa ya kitaifa kwa sasa ni siasa, kampeni za wagombea na vishawishi vyao. Lakini najua bado hamkosi elimu ya mapenzi na maisha.

Leo nataka kuwasaidia baadhi ya wanawake, hasa wasichana ambao wamejikuta wakiwa kwenye uhusiano usiodumu kwa sababu ya kuwapata wanaume wanaowatamani halafu wao kwa kutokujua, wakaamini wanapendwa. 

MAPENZI YALIVYO

Awali ya yote napenda kueleza kuwa, mapenzi yana hisia, yanagusa, yanagharimu. Wawili wanapotokea kupendana ndiyo huitwa mapenzi na si mmoja kupenda mwingine asipende. Huko ni kudanganyana. 

HALI ILIVYO

Lakini sasa kuna wanaume wanaopenda na wapo wasiopenda. Ila wanatamani. Mbaya zaidi kundi hili la wanaume wasiopenda bali wanatamani, hata wenyewe hawajijui kama hawajui kupenda. 

Baadhi ya wasichana wamekuwa wakilalamika kupigwa chini na wanaume. Tena wanasema hupatwa na kitendo hicho baada ya kukutana kimwili na wanaume hao mara moja au mbili. Msikie Jamila, mkazi wa Tandale, Dar:

“Mimi najiona nina mkosi. Mwanaume ananionesha ananipenda sana, nami najitoa kwake. Lakini akishalala na mimi mara moja au mbili, anaingia mitini. Hapokei simu, hajibu meseji. Nisaidie anko Ndauka.” 

KUNA HILI

Nisiseme tu kwamba tatizo la Jamila linatokana na kupata mwanaume anayetamani, lakini pia inawezekana ‘uwezo’ wake kwenye sita kwa sita unachangia. Wapo wanaume wakiona mwanamke ‘hajiwezi’ uwanjani, anamkimbia. Yaani mwanamke anakuwa hana sifa ya kumshika mwanaume. 

TURUDI KWENYE MADA

Hata hivyo, sasa turudi kwenye mada yetu ya leo; sifa tano za mwanaume anayekutamani. 

KUTODUMU NA MWANAMKE

Sifa ya kwanza ya mwanaume mwenye tabia hii ni kutokudumu na wanawake. Utakuta mwanaume ana mpenzi, baada ya mwezi mmoja wamemwagana, anakuwa na mwingine. Wapo wasiodumu na wapenzi wao hata kwa mwezi mmoja. 

KUKINAI TENDO LA NDOA

Sifa ya pili ya mwanaume mwenye tabia hii ni kukinai tendo la ndoa. Hapa namaanisha kuwa, mwanaume mwenye tabia ya kutamani huwa hawezi kukutana kimwili na mwanamke zaidi ya mara tatu. Anakuwa ameshamkinai na hamtaki tena. Chenga nyingi. Wako wengine, wenye sifa hii, akishamnasa mwanamke akalala naye mara moja tu, basi! Tena wengi wao wanapenda kuhifadhi kumbukumbu. 

Utakuta mwanaume anakuhesabia wanawake aliokwisha lala nao; Ester tayari, Jamila tayari, Jane pia, Suzana yeye juzijuzi tu. Halima zamani, Hawa tayari, sasa hivi namfukuzia Maimuna. Mwanaume wa hivi, anajua kutamani lakini si kupenda

Itaendelea toleo lijalo.
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...