WADAU WAFUNGUKA:WAMWAMBIA MAMA KANUMBA, UNAONAJE UKIACHANA NA LULU? ..SABABU HIZI HAPA

Admin Updates10 years ago4 Views


Ni miaka mitatu sasa tangu  kufariki kwa Steven Kanumba, mmoja kati ya
waigizaji mahiri waliojipatia mamia ya mashabiki kutokana na kazi zake
nzuri. Kwa watu wake wa karibu, na pengine mashabiki wote, kifo chake
kilikuwa ni cha ghafla na cha kushtua sana.


Kwa tuliomfahamu kiasi, huu siyo tena wakati wa kurejea maisha yake, kwa
sababu tulijua nini alitaka katika maisha yake ya uigizaji na kwa
kiwango kikubwa, alielekea kufanikiwa kulitangaza jina lake na nchi kwa
jumla katika uso wa kimataifa.


Hadi hapo sheria itakavyosema vinginevyo, tunaendelea kuamini kuwa kifo
chake kilikuwa ni makusudi ya Mwenyezi Mungu, kwamba kila nafsi itaonja
mauti, iwe kwa namna ambayo binadamu wataridhika au la. Wakati akifariki
dunia, usiku ule wa Aprili 6, 2012, Kanumba alikuwa chumbani na mpenzi
wake, Elizabeth Michael ambaye wengi tunamfahamu zaidi kama Lulu.


Lulu alikuwa bado binti mdogo wakati huo, kiasi kwamba hata baada ya
mamlaka kumkamata na kumuweka korokoroni, makundi mengi ya kijamii
yalimuonea huruma na haikushangaza alipotolewa rumande kwa dhamana. Ni
kweli alikuwa naye chumbani, ni kweli kulikuwa na mgogoro wa kimapenzi
baina yao na ni kweli pia kwamba alimuona Kanumba akianguka.


Lakini hatuwezi kumhukumu, kwa kuwa kesi ipo mahakamani, tusubiri maana tunaamini haki itatendeka.
Baada ya kifo chake, mama mzazi wa Kanumba, Flora Mtegoa amejitokeza na
kuwa ndiye mrithi wake. Ninajua mama huyu ndiye anahusika na vitu vingi
vya marehemu, zikiwemo mali zake.


Kwa kutambua kwamba kazi ya Mungu haina makosa, tangu mwanzo wa msiba,
mama Kanumba aliweka wazi kuwa hawezi kumhukumu Lulu, atampenda kama
mkwe wake kwa kuamini kuwa mwanaye alimpenda. Tumeshuhudia, familia hizi
mbili, ya Mama Kanumba na Mama Lulu wakiwa karibu zaidi kiuhusiano
kuliko wakati marehemu akiwa hai.


Binafsi, nimeshawahi kukutana nao, siyo mara moja au mbili, wazazi hawa
wawili wakiwa pamoja. Ni marafiki. Na mara kadhaa pia, Lulu ameonekana
akiwa pamoja na mama wa mpenzi wake, akisema wazi kuwa atamchukulia kama
mzazi wake.


Kijuujuu, tunatambua kuwa maisha yanaenda sawa kati ya familia hizo,
wakiishi kama ndugu na kwamba kifo cha Kanumba hakijaleta uhasama, jambo
ambalo ndilo muhimu zaidi.Lakini kauli ya mama Kanumba hivi karibuni,
aliyeongea kwa masikitiko juu ya kutupwa na Lulu, inapaswa kujadiliwa.
Kwangu mimi nadhani umma unapaswa kumsaidia mama huyu ili kumweka sawa
kisaikolojia, maana atakuwa na amani zaidi kuliko anavyoishi hivi sasa.


Sielewi anaposema Lulu amemtupa anamaanisha kutupwa kivipi, lakini kwa
namna walivyokuwa wakiishi, ni rahisi kwangu kujua kuwa analalamika kwa
vile binti huyo hivi sasa hamjali kama zamani alipomchukulia kuwa sawa
na mama yake mzazi. Alijitahidi kugawana naye chochote kidogo
alichopata.


Nimkumbushe tu mama kuwa siku zote, hisani zina mwisho. Na hata akigeuka
nyuma na kuangalia maisha baada ya mwanaye kufariki, atagundua kuwa
alipata misaada mingi mwanzoni, lakini kadiri siku zilivyokwenda,
ikapungua. Hii ndiyo ‘nature’ ya binadamu.


Kama Lulu alikuwa karibu naye wakati ule, ni kwamba  alitimiza wajibu
wake, kwanza kama mpenzi wa mwisho wa mwanaye na pili kama mtu
anayehusishwa na kifo hicho. Kibinadamu, alipaswa kufanya kama
alivyofanya. Lakini kutaka Lulu aendelee kuwa karibu, ni sawa na kumtaka
awe mtumwa.


Yule binti anahitaji maisha yake, yeye na familia yake. Litakuwa jambo
la ajabu sana kama mama Kanumba atategemea maisha yake kuendeshwa na
Lulu. Alijitahidi kadiri alivyoweza na kwa mtu mwenye busara, alipaswa
kumshukuru kuliko kumshutumu.


Ni vyema kumuacha huyu mtoto aendelee na maisha yake, ana watu wengi
nyuma yake. Ni dhambi, kumlaumu Lulu kwa maisha yoyote anayoishi mama
Kanumba kwa sasa, hizi ni changamoto ambazo Mungu aliamua kumuachia huyu
mama, azikabili!
GPL
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.