SOMO KWA WANAUME: TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA SULUHISHO LAKE

Admin Updates10 years ago6 Views

                    

Makala hii ni maalumu kwa ajili ya wanandoa tu na si vinginevyo au kama
elimu kwa wanandoa watarajiwa. Muogope Mungu uzinzi ni dhambi kubwa
sana.

Katika kilele cha mwisho kabisa cha furaha katika maisha ya ndoa, kama
inavyofahamika, ni sherehe inayopatikana katika tendo lenyewe la ndoa.
Hata hivyo, ili furaha ipatikane ni lazima tendo lenyewe lifanyike
katika hali ya afya kwa wanandoa.
Nguvu za kiume ni istilahi inayotumika mara nyingi
kurejelea ‘uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa’. Na inapokuwa
kinyume chake, tunasema ni ‘kupungua au kukosa nguvu za kiume’.
Kupungukiwa kwa nguvu za kiume hutofautiana. Inaweza kuwa ni kujumuisha
hali ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume, au hali ya kutokuwa na
uwezo wa kufika kileleni kwa muda mzuri wa kutosha.

Licha ya hivyo, elimu mhimu kabisa ambayo mwanaume anapaswa kuifahamu ni
kuwa, nguvu hizi hazitoki katika madawa ya kemikali au pahala pengine;
zinatoka katika vyakula tu.
Kwanini wanaume huishiwa nguvu za kiume?

Kuishiwa nguvu za kiume ni tatizo la kawaida kwa wanaume. Ni hali ya
kushindwa kwa uume kudumu kusimama barabara kwa ajili ya tendo la ndoa,
au kuwahi kufika kileleni.

Hatari ya kupungukiwa nguvu za kiume huongezeka kutokana na umri.
Kulingana na tafiti za kitabibu, wanaume wenye umri kuanzia miaka 60
tatizo hili ni kubwa kwao kuliko wanaume wenye umri wa miaka 40.

Wanaume wenye elimu ndogo juu ya utendaji kazi wa mwili na afya ndio
wanaokabiliwa sana na tatizo hili. Hii ni kwa sababu wanashindwa kuelewa
aina ya chakula kinachoongeza nguvu za kiume na za mwili kwa ujumla,
mtindo wa maisha wanayotakiwa kuishi ili kupunguza hatari hiyo,
wanakunywa pombe na hawafanyi mazoezi ya viungo. Mazoezi ya mwili
hupunguza hatari ya kupungukiwa nguvu za kiume. 

Tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume linaweza kuwa na sababu za kihisia
(emotional causes) lakini sababu nyingine hutokana na maradhi kama vile
kisukari na shinikizo la juu la damu.

Inakadiriwa kuwa asilimia 50 hadi 60 ya wanaume wenye maradhi ya
kisukari wana tatizo la uume kushindwa kusimama. Watu wanaosumbuliwa na
kiharusi na ulevi nao wana hatari kubwa sana kwa sababu ya uharibifu wa
korodani (testicles) kutokana na ulevi sugu na kupoteza testerone. Pombe
hupunguza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa manii (mbegu za kiume).

Watu wanaosumbuliwa na shinikizo la damu, magonjwa ya tezi, majeraha
(kama vile kutokana na upasuaji wa viungo vya uzazi), matumizi ya dawa
zenye kemikali bila mpangilio au ushauri wa wataalamu na maradhi ambayo
hudhoofisha mtiririko wa damu kwenye uume. Hata hivyo, upungufu wa nguvu
za kiume unatibika katika umri wa rika zote.

Kwa wenye maradhi kama hayo ni bora kwanza kuwaona wataalamu wa tiba.
Kwa ujumla, mtaalamu atafanya uchunguzi kimwili na maabara ya uchunguzi.
Hii itaruhusu yeye kupata kushughulika vizuri juu ya tatizo, hali
ambayo itamweka aendelee kutafiti chaguzi mbalimbali za tiba. Mhimu ni
lazima kushauriana na daktari kwa ushauri juu ya matibabu ambayo ni
bora.

Baadhi ya vipengele ambavyo daktari atahitaji kuvifahamu kabla ya kuanza
kukutibu tatizo la kuishiwa nguzu za kiume ni pamoja na;
  • Umri wa mgonjwa
  • Jumla ya afya kwa sasa
  • Utendaji wa tendo la ndoa zamani na sasa
  • Migogoro ya ndoa, kifamilia, kazi n.k
  • Ni nini malengo ya tiba ?

Kutafuta mtaalamu mzuri ni njia nzuri na ya kwanza katika kupata tiba
sahihi. Ni mhimu kwanza wewe kujisikia vizuri na kumwamini daktari wako,
kisaikolojia utakuwa umepiga hatua ya kwanza ya kupata nafuu ya maradhi
yanayokukabili.
Sababu zipi zinasababisha uume kushindwa kusimama?

Kushindwa kwa uume kusimama pia hujulikana kama kuishiwa nguvu za kiume.
Ni kitendo cha mtu kushindwa kusimamisha uume au kudumisha usimamaji wa
uume kwa muda wa kutosha kufanya tendo la tendo na mwenzake. Lakini
wakati hii inaweza kumfikisha mwanaume katika upeo wa raha (orgasm),
hali hii humwacha mwanamke akiwa hakuridhika. Mke wako hukutaka ukawie
ikiwezekana ukawie zaidi. Kama mwanaume hataweza kukawia, basi anakuwa
hampi raha mke wake.

Hata hivyo, kama una tatizo la kuwahi kufika kileleni hauko peke yako.
Takribani asilimia 30 hadi 40 ya wanaume wa rika zote wana tatizo hili.
Lakini vile vile kufahamu tu kuwa wanaume wengine pia wana tatizo kama
lako haitakusaidia kuondoa shida inayokukabili.

Habari nzuri kwa wanaume ikiwa ni pamoja na wewe ni kwamba kuna njia
zenye manufaa makubwa kabisa ya kumaliza tatizo hili na wakati huo huo
zikiwa ni rahisi sana.

Kuna wakati kushindwa kusimama uume kunaweza kuonekana kama si tatizo
lakini wakati hali hiyo inapoendelea kwa muda mrefu inaweza kuleta hisia
ya dhiki kubwa kwa mme na mke wake. Lakini hata hivyo, sababu za
kawaida zinazosababisha uume kushindwa kusimama ni pamoja na matatizo ya
mhemko kama vile;
  • Wasiwasi
  • Hofu
  • Msongo/Stress
  • Hasira
  • Huzuni
  • Ukosefu wa hamu katika mapenzi

Ili kuwa na uwezo wa uume kusimama panahitajika;
  1. Mfumo wa neva ulio na afya nzuri ambao unapeleka mpwito neva (nerve impulses) katika ubongo, uti wa mgongo na uume.
  2. Mishipa ya ateri iliyo na afya ya ndani na iliyo karibu na corpora cavernosa
  3. Misuli laini yenye afya na tishu za ufumwele (fibrous tissues) ndani ya corpora cavernosa na
  4. Kiwango sahihi cha oksidi nitriki (nitric oxide) ndani ya uume.

Kushindwa kwa uume kusimama kunaweza kutokea kama kipengele kimojawapo
katika hivyo vilivyotajwa hapo juu hakipo. Pia sababu zingine za
kupunguwa kwa nguvu za kiume, kushindwa kwa uume kusimama, au kuwahi
kufika kileleni ni pamoja na;
  • Umri
  • Maradhi ya kisukari
  • Kujichua/Punyeto
  • Uzinzi
  • Ukosefu wa Elimu ya vyakula
  • Kutokujishughulisha na mazoezi
  • Shinikizo la juu la damu
  • Maradhi ya moyo
  • Uvutaji sigara/tumbaku
  • Utumiaji uliozidi wa kafeina
  • Kudhurika kwa neva au uti wa mgongo
  • Madawa ya kulevya kama vile bangi, heroini, kokeini, na pombe
  • Kiwango kidogo cha testerone
  • Kuumia kwa kinena (groin) au kuharibika
  • Athari
    kutoka kwa baadhi ya dawa ikiwa ni pamoja na madawa ya kwa ajili ya
    kutibu huzuni, maradhi ya moyo, shinikizo la damu na kifafa (epilepsy)
    na kadharika. Na madawa kama vile; Estrogen, Antiandrogens (flutamide),
    Lupron, Proscar, Diuretics, Methyldopa, Beta blockers, Calcium channel
    blockers, Tranquilizers (vitulizaji), Decongestants, Seizure
    medications, Madawa ya kupunguza kolesto, Cimetidine (dawa ya vidonda
    vya tumbo), Digoxin na kadharika.
Uhusiano wa nguvu za kiume na mzunguko wa damu:
Nini kinachofanya uume usimame? Kwa haraka unaweza kujibu ni msisimko. Naam, unaweza kuwa sahihi. Lakini msisimko ni matokeo. Kuna kinachosababishamsisimko huo. Bila hicho, msisimko hauwezi kutokea.

Kila mwanaume anapaswa kuwa na jibu sahihi la swali hili, ili atakapoona
tatizo ajuwe pa kuanzia na pa kumalizia. Hata kama si kwa undani, Elimu
ya kujijuwa jinsi mfumo wako wa mwili unavyofanya kazi ni mhimu sana
kwa kila mtu na si kwa madaktari pekee kama ilivyo dhana ya watu wengi.

Kutokuwa na chochote kichwani kuhusu miili yetu ndiyo sababu kubwa
inayotufanya kuparamia madawa kiholela na hivyo kujidhuru badala ya
kujitibu.

Kinachofanya uume usimame ni mzunguko wa damu. Na kabla hujaendelea
kusoma tambua jambo moja mhimu; ‘’Asilimia 94 ya damu ni maji’’. Hii ni
kusema katika kila lita 10 za damu, lita 9 kati ya hizo 10 ni maji. Kwa
kifupi maji ndiyo kila kitu mwilini na kama bado unasubiri kiu ndipo
unywe maji na tena unakunywa maji ya baridi ya kwenye friji, POLE SANA

Mzunguko wa damu unaofanya kazi vizuri kama inavyotakiwa na usio na
hitilafu yeyote ni kipengele mhimu sana katika kusimama kwa uume wako.
Kwanini?
Mzunguko wa damu ulio katika afya njema
husambaza damu ya kutosha katika viungo vyako vyote vya mwili wako ikiwa
ni pamoja na kwenye mishipa ya uume wako. Hii ni kwamba hata kama
utagusana na mwanamke hautaweza kufanya chochote kama damu haizunguki
katika viungo vyako inavyostahili. Tazama mtu aliyekufa, damu
haizunguki, je anafanya chochote? Hata hivyo huo ni mfano wa juu zaidi.

Ina maana kwamba, chochote ambacho huzuia mtiririko wa damu kwenda
kwenye uume kinaweza kuzuia kusimama kwa uume. Kama mishipa yako ya vena
na ateri imeziba, mwili wako hautaweza kusimamisha uume. Hii ni kwa
sababu uume hautapata damu ya kutosha.

Mara nyingi vena zilizoziba sababu ya mzunguko dhaifu wa damu ni sababu
ya kushindwa kusimama uume kwa wanaume walio na umri zaidi ya miaka 60,
wanaume wenye kisukari na pia wanaume wenye ateriosclorisis (hali ya
ugonjwa inayosababishwa na kukauka kwa vijiateri vya ateri), na wenye
maradhi ya moyo.

Kwa watu wengi, sababu ya kuishiwa nguvu za kiume ni mlo wa mafuta mengi
ambayo yanaweza kuzuia mtiririko mzuri wa damu kwenye uume. Inashauriwa
pia kuepuka vinywaji na vyakula vilivyosindikwa viwandani.

Katika tendo la ndoa kwa mwanaume, mishipa ya ateri ina nafasi kubwa
sana kutokana na kazi yake ya usafirishaji wa damu kwenda sehemu
mbalimbali za mwili, hivyo unashauriwa kujifunza namna ya kutunza ateri
za mwili wako ili kuruhusu mtiririko mzuri wa damu mwilini mwako.

Pia ni jambo la busara sana kuwaona wataalamu wa tiba kuhusu
unavyojisikia na jinsi unavyohisi kuwa pengine unaweza kuwa na tatizo
katika mishipa yako ya ateri. Jaribu kujenga utaratibu wa kuwa
unajichunguza mara kwa mara kama utahisi kunyemelewa na tatizo hili.
Baadhi ya watu hufanya maradhi kuwa sugu kwa sababu ya kutopendelea
kujichunguza mara kwa mara hadi wauguwe taabani, huku ni kukosa kuelewa
na kushindwa kujithamini mwenyewe.
Jitibu tatizo la kupungua nguvu za kiume:

Katika kujitibu tatizo hili jambo la kwanza ni kuelewa ni nini kimesababisha tatizo hilo kwa upande wako.

Ikiwa unasumbuliwa na mfadhaiko/stress uangalifu mkubwa unahitajika
kabla ya kuamua kutumia dawa yoyote. Katika hali ya mfadhaiko wa akili
utokanao na hali ya kushuka kwa uchumi kwa mfano, wanandoa wanapaswa
kuwa ni wenye umoja na kujaliana zaidi, shida ni pale kama mke akili
yake ni ndogo kwani badala ya kufunga na kuomba huenda akaenda
kukutangaza kwa majirani!. 

Kama tatizo limesababishwa na magonjwa kama kisukari, shinikizo la juu
la damu au uzito kupita kiasi ni vema ukajitibu kwanza na maradhi haya.
Tatizo ni kuwa watu wameaminishwa kwamba maradhi haya hayana dawa jambo
ambalo si kweli, kisukari, shinikizo la damu na hata uzito ni magonjwa
yanayotibika kabisa hasa kwa kutumia dawa mbadala na kufuata muongozo
sahihi katika kula na kunywa kwa kipindi cha majuma kadhaa.

Kama tatizo linatokana na matumizi ya vilevi, hatua ya kwanza ni
kuviacha kwanza hivyo vilevi. Ndiyo kuviacha kwanza, unatakiwa ujiulize
mwenyewe kipi ni mhimu kwako ndoa yako au hivyo vilevi? Mtu anayejali
vilevi kuliko hata afya yake hafai. Na kanuni ni hii; ukitaka uzuri ni
lazima udhurike kwanza. Kuna watu wanajidanganya kwamba ukitumia sijuwi
kilevi fulani nguvu zinaongezeka, ni kweli zitaongezeka hapo mwanzoni
mwa matumizi ya hicho kilevi lakini kadri siku zinavyoenda ndivyo
utakavyoendelea kuwa mtegemezi wa hicho kilevi na itafika siku hata
hicho kilevi hakitasaidia kitu na hapo ndipo hatari zaidi ya kutotibika
tatizo lako itakapojitokeza.

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...