ROSE NDAUKA NA SHETTA WADAIWA KULALA CHUMBA KIMOJA HOTELINI ..HABARI YOTE HII HAPA

Admin Updates10 years ago4 Views


KIMESANUKA! Mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nurdin Bilal maarufu
kama Shetta anadaiwa kulala chumba kimoja na staa wa filamu Bongo, Rose
Ndauka katika hoteli iitwayo Kingway iliyoko mkoani Morogoro mwishoni
mwa wiki iliyopita.

Chanzo makini kinachofahamu kwa undani kinachoendelea baina ya mastaa
hao wawili, kimelidokeza gazeti hili kuwa tukio hilo lilijiri wakati
wakielekea katika shughuli za mazishi ya muasisi wa Kundi la Tip Top
Connection, Abdul Bonge aliyezikwa kijijini kwao Mkuyuni mkoani humo,
ambako watu wengi maarufu walihudhuria.

“Si unajua mastaa kibao walikuwepo kwenye ule msiba, basi Rose na Shetta
nao walikuwepo na wakati wa kwenda Mkuyuni, walipanda gari la Shetta
hadi Morogoro mjini ambako walichukua chumba na kulala wote hadi kesho
yake walipohudhuria mazishi na kurejea Dar es Salaam,” kilisema chanzo
hicho.

Ili kushibisha maelezo yake, mtoa habari huyo alilitumia gazeti hili
video ya wawili hao wakiwa ndani ya gari la Shetta inayomuonyesha Rose
akiimba nyimbo mbalimbali za mkali huyo anayetamba na kibao chake kipya
cha Shikorobo ambacho video yake imefanywa na mtayarishaji anayetamba
nchini kwa sasa, Godfather wa Afrika Kusini.

Hata hivyo, haikuweza kufahamika mara moja kama uhusiano wa wawili hao
ni wa siku nyingi au umeanza hivi karibuni, ingawa gazeti hili
linafahamu kuwa Shetta ni mume wa mtu akiwa amezaa naye mtoto mmoja.
Amani lilimtafuta Shetta na kufanikiwa kumpata kwa njia ya simu yake ya
mkononi na aliposomewa mashtaka, kwanza alicheka na kusema kuwa ni kweli
alikuwa msibani na alirejea Dar akiwa na Rose katika gari lake.

“Ninachoweza kusema ni kuwa ni kweli nilimpa lifti Rose wakati tunaenda
kwenye mazishi ya Bonge. Kulikuwa na magari mengi ambayo mtu yeyote
angeweza kupata lifti na ni kweli pia tulilala Morogoro, ilikuwa ni
hoteli moja lakini kila mtu alilala chumba chake, siwezi kujihusisha na
hayo mambo, mimi nina familia,” alisema msanii huyo ambaye pia aliwahi
kutamba na kibao cha Kerewa, alichomshirikisha Diamond.

Kwa upande wake, Rose Ndauka alipoulizwa kuhusu suala hilo, kwanza
alishtuka na kuuliza zilikopatikana habari hizo kabla ya kukiri ukweli
kuwa alipanda gari la Shetta na wote kulala hoteli moja mjini Morogoro,
lakini kila mtu na chumba chake.

“Halafu nisingependa kuandikwa andikwa kila siku kwa mambo hayo, unajua
kama mimi nina mtu wangu? Andikeni halafu tutaonana mahakamani, maana
naona lengo lenu ni kuniharibia,” alisema Rose
GPL

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.