Taarifa ya NSSF kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana Januari 6,2019 imesema Mfuko unaendelea kupokea na kuhakiki madai mbali mbali kutoka kwa wanachama ambao ajira zao zimekoma na walikuwa kwenye ajira za muda maalumu kwenye sekta mbali mbali kama vile madini, viwanda, ujenzi na kilimo.
Imesema madai yote yanayothibitishwa kuwa ni halali baada ya kuhakikiwa, mwanachama atalipwa mafao yake. Meneja Kiongozi wa Matekelezo (Chief Manager Compliance and Data Management ) Cosmas Sasi amesema NSSF inaendelea kulipa mafao mbali mbali kwa wanachama wake kwa wakati. Kwa upande wa mafao ya uzeeni takribani Sh. bilioni 5 zimekuwa zinalipwa kila mwezi kwa wastaafu wetu kuanzia julai 2018.Wakati kwa pensheni ya Desemba,2018 Sh. Bilioni 4.83 kimeshalipwa kwa wastaafu 18,631 walikuwepo kwenye daftari la wastaafu.
Kwa upande wa malimbikizo ya mafao hadi kufikia julai 2018 jumla ya Sh. bilioni 108 zilikuwa zinadaiwa kwenye Shirika, ambapo kiasi cha Sh. bilioni 85 kimelipwa kwa wanachama waliokuwa na madai mbali mbali baada ya uhakiki kukamilika, kiasi kilichobaki cha sh. bilioni 23 kitalipwa baada ya uhakiki unaondelea kukamilika.
Wakati huo huo Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa UmaLulu Mengele amesema Mfuko ulianza mchakato wa kuhakiki wastaafu wake kuanzia Desemba 1, 2018 na bado unaendelea kwenye ofisi mbali mbali za NSSF zilizoko mikoa yote ya Tanzania Bara .”Wastaafu ambao hawajajitokeza kuhakiki, wanaombwa wafike kwenye ofisi zetu 65 zilizoko katika maeneo mbali mbali katika mikoa yote Tanzania bara kwa upande wa wastaafu wanaoishi Zanzibar watahakikiwa kwenye ofisi za ZSSF.
“Madai yote yanayothibitishwa kuwa ni halali baada ya kuhakikiwa, mwanachama atalipwa mafao yake. kwa hiyo NSSF kwa sasa inaendelea kulipa mafao mbali mbali kwa wanachama wake kwa wakati,”,alisema Lulu.Pichani kushoto ni
Meneja Kiongozi wa Matekelezo ,Cosmas Sasi Kutoka Shirika NSSF.from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2RsM18T
via