Mara baaba ya kipindi cha nyuma kutibuana, kwa mara ya kwanza Harmorapa amezungumzia uhusiano na Dudu Baya ulivyo kwa sasa.
Harmorapa ameeleza kuwa anamjua vizuri Dudu Baya ingawa hawajawahi kukutana wala kuwasiliana na ugomvi wao ulikuwa kwenye mitandao tu.
“Konki, kwanini nisjimjue nikisema simjui nitakuwa najichumia dhambi hata kwa Mungu, kama inafikia hatua ya kunizungumzia ina maana anajijua na mimi namjua yeye nani,” ameeleza Harmorapa.
Utakumbuka mara baada ya Harmorapa kuingilia kati kitu ambacho Dudu Baya alikiita ni vita dhidi ya ushoga, Dudu Baya alihaidi kumpatia kichapo msanii huyo mwenye matukio ya aina yake kwenye muziki.
from UDAKU SPECIAL BLOG http://bit.ly/2W1xnEP
via