
Mwanamuziki Aslay Isihaka kutoka katika kundi la Yamoto Band amefunguka
na kuweka wazi kuwa anasumbuliwa sana na watoto wa kike ndiyo maana
ameamua kuweka mahusiano yake wazi, Aslay alifunguka hayo alipokuwa akichat Live katika kipengele cha Kikaangoni Live kinachofanyika kila
siku ya Jumatano, kuanzia saa nane mchana mpaka kumi Alasiri kupitia
ukurasa wa facebook wa EATV.
Aslay alisema kuwa moja ya sababu iliyomfanya kumuweka wazi mpenzi wake
huyo ni kutaka kutoa ujumbe kwa wale ambao wanamsumbua kuwa waache
kufanya hivyo kwani tayari ana mtu ambae yeye anampenda.
“Nimeamua kuweka mahusiano yangu ya mapenzi wazi sababu nasumbuliwa
sana, nahisi kufanya hivyo wataelewa na kuacha, yaani kama
nimewapunguzia speed ya usumbufu”
Mbali na hilo Aslay aliweza kuzungumzia juu ya elimu yake na kusema
hakuacha shule kwa sababu ya muziki ila ataendelea na shule pale
alipoishia, ilaa anaamini atafanya hivyo siku za usoni.
YAMOTO BAND
Mkali huyo ambaye amejipa jina la dingi mtoto amesema kuwa hafikiri
kuondoka Yamoto band wala hawazi suala hilo, ila amesema kuwa kwa sasa
yeye na wenzake wanajipanga kufanya kazi za kimataifa hivyo wanasubiri
majibu kutoka kwa Yemi Alade, kwa kazi ambayo wamemtumia hivyo pia
ameeleza kuwa kuna kazi ambayo wamefanya na Sauti Soul wa nchini Kenya
ambao waliwaomba kufanya nao kazi.
MAHUSIANO YAKE NA WEMA
Tetesi zilizopo mtaani ni kwamba Aslay Isihaka alikuwa akifukuziwa na
Wema Sepetu kimapenzi na watu wengi walipouliza swali walitaka kufahamu
ukweli juu ya suala hilo na ndipo hapo Aslay alipofunguka na kuweka wazi
juu ya suala hilo na kusema kuwa hakuna ukweli wowote na wimbo wa
Nitakupwelepweta hajaimbiwa Wema Sepetu.
“Watu wanakuwa wanaongea mambo mengi juu ya maisha yangu hususani katika
mahusiano na kusambaza taarifa zisizo na ukweli, mfano watu wanasema
natoka kimapenzi na Wema huo siyo ukweli kabisaa bali Wema ni kama dada
yangu, ila kutokana na mambo haya ndipo niliamua kuweka mahusiano yangu
wazi ili kila mtu ajue kuwa nipo kwenye mahusiano na mtu fulani na
waache kusambaza taarifa zisizo na ukweli.”
Kwa kifupi hizo taarifa wanazosema mashabiki hazina ukweli wowote,kwa
sasa nimemtangaza mpenzi wangu na ndiye niko nae, sitaki usumbufu tena
kwa sasa.