MWIGIZAJI JOHARI AMKANA RAY LAIVU!..KISA?..SHUHUDIA MWENYEWE

Admin Updates10 years ago6 Views



Staa wa Bongo Movies na mmiliki mwenza  wa kampuni ya filamu nchini ya
‘RJ Company’, Blandina Chagula ‘Johari’, ameibuka na kushangaza wengi
kwa kauli yake kwamba hakuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na
mwigizaji mwenzake, Vicent Kigosi ‘Ray’.

Staa huyo aliwahi kukiri kuwa na uhusiano huo na msanii huyo na kwamba
walishaachana kwa amani, ndiyo maana waliweza kuendelea na kampuni yao
ya masuala ya filamu ya Rj Company.

Juzi Johari ameliambia gazeti la Mtanzania kwamba, muda mrefu alikuwa
akisikiliza wanaodai hana uelewano mzuri na Ray kutokana na kuwa na
uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji Chuchu Hans na sasa ameamua kuweka
wazi suala hilo.

“Ni kwa kipindi kirefu sana yamezuka maneno yanayodai mimi na Ray
tulishawahi kuwa wapenzi, kitu ambacho si cha kweli, tena kibaya zaidi
wameongeza kuwa hatuna maelewano mazuri kikazi,” alieleza Johari.
Aliendelea kufafanua: “Sikuwahi kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi kama
wengi wanavyofikiria na kama ningekuwa na uhusiano wa kimapenzi na Ray
na tumeachana, hata kampuni yetu ingeshavunjika kwa kuwa tungekuwa na
chuki, nawaambia hatutegemei kutengana kikazi wala kirafiki,” alisema
Johari

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.