Viongozi wa nchi hizo, akiwamo Yoweri
Museveni (Uganda), Paul Kagame (Rwanda) na Uhuru Kenyetta wa Kenya,
wanadaiwa kuanzisha umoja wa hiari, huku wakifanya vikao vya siri na
kuitenga Tanzania.

Akizungumzia hali hiyo, Balozi
Mwapachu alisema amewahi kuandika mambo mbalimbali juu ya EAC na dalili
za kutokea migogoro inayotokea sasa, lakini hakuna hatua zilizochukuliwa
za kudhibiti.

Hata hivyo, Mwapachu hakuweza kueleza
ni mahali gani alitoa ushauri upi kuhusu jumuiya hiyo, zaidi ya
kusisitiza kuwa amechoshwa na migogoro ya chombo hicho.

“Niseme nini mimi, sina la kuzungumza,
nimeshaandika sana, nimeshauri sana, na sasa nimechoka, siwezi tena
kusema lolote,” alisema Balozi Mwapachu, bila kufafanua zaidi na baadaye
kukata simu.

Wakati Mwapachu akionekana kuchoshwa
na kinachotokea ndani ya EAC, dalili za wazi za kuvunjika kwa jumuiya
hiyo zimeanza kuonekana.

Kwa muda sasa marais hao wanakutana
kuweka mikakati ya siri bila kuzishirikisha nchi za Tanzania na Burundi,
ambapo mapema wiki hii, walimwalika Rais wa Sudan Kusini, Silva Kiir,
kwenye mkutano wao.

Hali hiyo imeonekana kuwakera wabunge
wa Bunge la Tanzania wanaoendelea na kikao chao mjini Dodoma na
kushinikiza wapewe ufafanuzi wa kinachoendelea.

Akitoa hoja ndani ya Bunge, Mbunge wa
Same Mashariki, Anne Kilango, alisema jumuiya hiyo ipo hatarini
kuvunjika na kutaka Tanzania isiendelee na shughuli nyingine yoyote
inayoihusu jumuiya hiyo, hadi pale hatima yake itakapojulikana.

Mbunge wa Viti Maalumu (CUF), Rukia
Ahmed, naye aliitaka serikali kupeleka bungeni pendekezo la kujitoa
katika jumuiya hiyo, ili wabunge walipitishe.

Akijibu hoja hizo, Waziri wa
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, alisema Tanzania imeanza
mazungumzo na nchi za Burundi na Congo DR, kuangalia namna ya kuwa na
ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo.

Hata hivyo, Sitta alisema Tanzania
haiwezi kuamua lolote kwa sasa, hadi itakapopata taarifa ya kina kuhusu
mikutano ya mara kwa mara inayofanywa na viongozi wa nchi tatu za
jumuiya hiyo.

Mkutano wa kwanza wa viongozi hao
ambao hawakuishirikisha Tanzania, ulifanyika ghafla Entebbe (Uganda),
Juni, mwaka huu, ukafuatiwa na mkutano wa Mombasa (Kenya) Agosti 28 na
juzi wakuu hao walikutana Kigali, Rwanda.

Akielezea msimamo wa Tanzania kwa
wabunge juzi, Waziri Sitta alisema Tanzania haiwezi kupewa talaka katika
jumuiya hiyo, kwa kuwa ina eneo la zaidi ya asilimia 52 ya eneo zima la
EAC na asilimia 48 iliyobaki nchi nyingine zinagawana.

Hata hivyo, alisema ingawa Kenya,
Uganda na Rwanda hawajaanzisha rasmi jumuiya yao, dalili zinaonesha kuwa
wapo katika harakati ambazo hatima yake haijulikani.

Kwa muda mrefu sasa, mgogoro
unaofukuta ndani ya jumuiya hiyo umewalazimisha wadau mbalimbali wa
uchumi na siasa nchini kuitaka serikali kuachana na EAC na kuelekeza
nguvu zake zaidi katika Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa
Afrika (SADC).Chanzo: mtanzania