MTANGAZAJI GARDNER ATAKA JIDE AELEZE UKWELI JUU YA NDOA YAO,ANGALIA HAPA

Admin Updates10 years ago4 Views

JIDEE

Habari ya mjini katika ulimwengu wa mastaa Bongo ni kitendo cha
mtangazaji mwenye jina kubwa wa Kipindi cha Maskani cha Redio Times FM,
Gardner G Habash ‘Kepteini’ kutaka mwanamuziki Judith Wambura Mbibo
‘Jide’ ndiye aeleze ukweli juu ya ndoa yao.

Mtangazaji wa Redio Times FM, Gardner G Habash ‘Kepteini’
Akizungumza kwenye Kipindi cha Mkasi kinachorushwa hewani kupitia
Televisheni ya EATV chini ya ‘hosti’ wake, Salama Jabir, Jumanne
iliyopita, Gardner
alikataa kuzungumzia ndoa yake inayodaiwa kuvunjika.
 

Pamoja na mambo mengine ambayo aliyajibu kwa ufasaha, Gardner
alipoulizwa juu ya habari zinazozungumzwa mtaani kuhusu kuvunjika
uhusiano wake na Jide au Lady Jaydee, aligoma kulizungumzia kwa kigezo
kwamba kipindi hicho kilimhusu yeye tu.
Mwanamuziki wa Bongo fleva kitambo, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’
Mtangazaji huyo alikwenda mbele zaidi kwa kumwambia Salama kwamba
amwite Jaydee kwenye kipindi hicho ili alielezee jambo hilo kwa
undani.Gardner na Jaydee ambao walifunga ndoa mwaka 2005, wamekuwa
wakidaiwa kuwa hawapo pamoja tena huku majukumu ya mtangazaji huyo
ambaye alikuwa meneja wa mwanamuziki huyo yakielea. Kipindi chake
cha Diary of Lady Jaydee kilichokuwa kikisimamiwa na Gardner ambacho
sasa anakiongozwa na ndugu wa msanii ndugu yake aitwaye Wakazi, Jumapili
iliyopita Jidealionekana kwenye harusi ya ndugu yake aitwaye Lameck
Mbibo aka Dabo ambaye pia ni msanii wa Dance Hall akiwa bila mumewe kama
ilivyozoeleka.







Source: baabkubwa magazine

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.