Musa Mateja
Mara baada ya kuelezwa
kwamba wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi huku wenyewe wakidanganya wana
‘projekti’, hatimaye majirani wamefichua kuwa mwigizaji Shamsa Ford na
mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay’, sasa wanaishi kama mke na mume.Mwigizaji Shamsa Ford na mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay’ wakizungumza jambo.
Baada
ya kutonywa ‘mchapo’ huo, gazeti hili liliwadamkia nyumbani kwa Nay
maeneo ya Kimara-Korogwe jijini Dar na kumkuta Shamsa akiwa na kanga
moja.Mwanahabari wetu, baada ya kufika nyumbani hapo mishale ya asubuhi
alikuwa bega kwa bega kuwafuatilia ambapo alifanikiwa kugundua kwamba
wawili hao sasa wanaishi kama mume na mke.
Habari zilizopatikana
zilidai kwamba, kwa sasa Shamsa hana muda mwingi wa kukaa nyumbani kwake
kwani asilimia tisini kama si mia moja kabisa, anautumia kukaa na Nay
nyumbani hapo.Mara kadhaa mwandishi wetu amekuwa akifika nyumbani hapo
na kumkuta Shamsa akipika na kupakua huku akiwa na kanga moja huku
wenyewe wakiitana mke na mume na kuoneshana mahaba motomoto..