MSANII MAMA ABDUL AWACHARUKIA WALIOSUSIA KITABU CHA KANUMBA

Admin Updates10 years ago7 Views

Muigizaji mkongwe nchini, Salome Nonge ‘Mama Abdul’.


Na Deogratius Mongela /UWAZI
MUIGIZAJI mkongwe
nchini, Salome Nonge ‘Mama Abdul’ amewacharukia mastaa wa filamu Bongo
kwa kususia kujitokeza katika uzinduzi wa kitabu cha Kanumba.



Akizungumza na Uwazi, Mama Abdul aliyasema hayo muda mfupi baada ya
kuisha kwa uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika mwishoni mwa wiki
iliyopita katika Ukumbi wa Landmark, Ubungo Riverside ambapo
alisikitishwa kutokana na marehemu kuwa mchango mkubwa katika tasnia ya
filamu.



“Wasanii wetu ni wanafiki, wanapata wapi jeuri ya kumtenga Mama Kanumba
wakati kwenye msiba walikuwa wote? Au tuseme wameona kwenye uzinduzi
hakuna namna ya kupiga dili kama walivyozoea watawakosa watu wa kuwauzia
sura.”
Mama Kanumba( wa tatu kulia) akiwa na wadau waliojitokeza katika uzinduzi wa kitabu cha Kanumba.



“Wamenikera, halafu wakimuona Mama Kanumba wanajifanya kumsalimia
kinafiki. Bongo hakuna kama Kanumba waache kujishauwa,” alisema Mama
Abdul.

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...