MSANII JACK PATRICK ANENA MAZITO AKIWA JELA – CHINA, NI KUHUSU ZARI NA DIAMOND,NA USALITI WA JUX KWA VANESSA….

Admin Updates10 years ago6 Views


Wakati akiendelea kutumikia kifungo akiwa jela huko Macau, Hong Kong
nchini China, modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff  ‘Jack
Patrick’ amenena mazito juu ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na
mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Juma Khalid ‘Jux’,
Vanessa Mdee, Aunt Ezekiel na Moze Iyobo.

Modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff  ‘Jack Patrick’.


BARUA KUTOKA CHINA
Jack
aliyekamatwa nchini humo kwa msala wa madawa ya kulevya ‘unga’ mwaka
2013 kisha kufungwa miaka sita kwenye Gereza la Macau, hivi karibuni
alilitumia gazeti hili barua nzito akionesha kushtushwa na vitu fulani
vya mastaa hao.

MIMBA YA AUNT
Moja
kati ya mambo yaliyomshtua Jack ni mimba ya mwigizaji Aunt Ezekiel
ambaye ni mke wa mtu, Sunday Demonte anayodaiwa kupachikwa na mcheza
shoo wa Diamond, Moze Iyobo.
Hata hivyo, katika skendo hiyo, Jack aliwataka watu wamuache Aunt apumzike kwani mapenzi hayachagui hasa kama ana furaha.

Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Wema Sepetu.


“Nimeshtushwa na udaku special Lol! Sasa Aunt ameamua kutulia na
Iyobo…acha apumzike mapenzi hayachagui as long as ndiyo furaha yake,
that’s okey,” aliandika Jack.

DIAMOND, ZARI
Mbali
na mimba hiyo ya Aunt inayoelekea kuzaa matunda muda si mrefu, modo
huyo alionesha kushtushwa na penzi la staa wa Bongo Fleva, Diamond
Platnumz na Zari akishangaa ilikuwaje hadi jamaa huyo akaachana na Wema
Sepetu kisha kutua kwa mrembo huyo mwenye maskani yake nchini Afrika
Kusini na Uganda.


“Heh! Kwani Diamond aliachana na Wema tena?” Alihoji Jack na kuongeza:
“Sasa
Zari si anakaa South Africa ‘Sauzi’? Wanaonana vipi na Platnumz? Mh!
Wala hawatadumu maana mapenzi ya mbalimbali. Labda kama Nasibu (Diamond
Platnumz) atahamia South.

Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ wakiwa kwenye pozi.

KAJALA Vs WEMA
Pia
video queen huyo wa Ngoma za Nataka Kulewa (ya Diamond), She Got A Gwan
(ya Marehemu Ngwea) na Kamugisha (ya Linex) aliulizia lile bifu zito la
Wema na Kajala Masanja kama lilikwisha kwani mastaa wa Bongo Movies
walishazoeleka kugombana na kupatana.


Bifu hilo ni lile la Wema kumtuhumu Kajala kumchukulia bwana’ke (CK)
huku akisahahu kwamba alimlipia Sh. Milioni 13 ili asiende jela miaka
mitano baada ya kukutwa na hatia ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.“Ya Kay (Kajala) na Wema naona
mwishowe watarudisha urafiki tu. Ya Bongo Movies nimeshayazoea huwa
wako hivyo kila muda, kawaida yao.”


JUX, VANESSA
Jack alipofika kwenye ishu ya kusalitiwa na staa wa
Bongo Fleva, Jux akidaiwa kuwa kwenye malovee na sexy lady wa muziki wa
Kizazi Kipya, Vanessa ‘Vee Money’, aliandika ishu hiyo kwa hisia zaidi
huku akijilaumu mwenyewe kwa kosa alilofanya.

Juma Khalid ‘Jux’, akiwa na mpenzi wake Vanessa Mdee.


“Ya Jux na Vanessa nimeamua tu kuyaacha coz nipo jela siwezi kumzuia
kufanya lolote then ni makosa yangu yaliyofanya hayo yote kutokea.“Sijui
hata kama itakuja kutokea tena kuwa wote tena mimi na yeye, that
chapter closed already, nahesabia muda mfupi tu now nitatoka lakini sina
chochote cha kufanya nionane naye,” alimalizia kuandika Jack.


Jack Patrick alihukumiwa kifungo hicho mwaka jana lakini taarifa
zilieleza kuwa endapo ataonesha nidhamu gerezani ataachiwa mapenzi hivyo
hatakaa jela miaka yote sita.

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.