Mkurugenzi wa Dar24 Apatikana Kigambo Mbuyuni..Asimulia Kilichotokea

Admin Updates7 months ago7 Views

Mkurugenzi Mtendaji wa Television inayotoa habari mitandaoni ya Dar 24 Media ambaye pia ni Mtendaji wa Data Vision aitwaye MacLean Godfrey Mwaijonga ambaye alipotea tangu October 31,2024 alipotoka ofisini saa 11 jioni, amepatikana jioni ya leo November 02,2024 eneo la Buyuni Wilayani Kigamboni Jijini Dar es salaam
Akiongea usiku huu mbele ya Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es salaam Jumanne Muliro na Familia yake Central Police Dar es salaam, MacLean amesema hakutekwa maeneo ya ofisini kwake bali alienda mwenyewe Kigamboni kukutana na Wafanyabiashara wenzake anaowafahamu ili wafanye maongezi ya kibiashara lakini wakamuwekea dawa ya kulevya kwenye juisi na akapoteza fahamu na alipozinduka wakaanza kumshinikiza awape password za benki na za mitandao ya kampuni anazozisimamia “Walinitoa waliponiweka sipafahamu na wakaniweka kwenye gari wakidai walichotaka niwape walipoona hawapatii wakaniacha Buyuni”
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Muliro Jumanne Muliro amesema kuwa taarifa za kupatikana kwa MacLean alizipata kutoka kwa Baba Mzazi wa Kijana huyo ambaye alipigiwa simu na Msamaria mwema kuwa wamemkuta Mac Buyuni ambapo alitelekezwa na wenzake na wakiwa na Ndugu zake walienda mpaka maeneo ya Kigamboni, Buyuni na kumkuta akiwa barabarani anapepesuka kisha walimpeleka Hospitali na baada ya vipimo ilionekana ana afya njema.
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.