Mr and Mrs Mengi wakiwa na furaha siku ya Ndoa yao Mimi Dr. Reginald Mengi naahidi kumpenda Jacqueline Ntuyabaliwe katika shida na raha hadi kifo kitutenganishe Ilikuwa ni furaha, upendo wa dhati na shangwe pomoni.
Baada ya miaka kadhaa ya uhusiano thabiti na uliokuwa umetawaliwa na
upendo usio kifani, Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Limited, Dr. Reginald
Mengi na Miss Tanzania, 2000, Jacqueline Ntuyabaliwe wamefunga
ndoaWawili hao wamebahatika kupata watoto wawili mapacha pamoja. Watoto
hao wa kiume nao waliungana na wazazi wao kushuhudia wazazi wao
wakibadilisha viapo vya ndoa. Watoto
mapacha wa Dr. Mengi na K-Lynn wakiwa wamebeba pambo maalum
lililoandikwa maneno ya Kiingereza yanayomaanisha ‘Karibu Bibi Harusi’ Dr.
Mengi na Jacqueline anayefahamika pia kwa jina la K-Lynn, walifunga
ndoa mwishoni mwa mwezi uliopita katika harusi iliyofanyika nchini
Mauritius. Bibi Harusi Jacqueline Ntuyabaliwe akitembea kwa hatua za kinyonga kujongea mbele ya mashahidi na tayari kwa kusema ‘Yes I do’ Harusi hiyo ya aina yake ilihudhuriwa na watu takriban 50 ambao wengi wao ni ndugu na marafiki zao wa karibu. Mr.
and Mrs. Mengi wakiwa kwenye picha ya pamoja na wana familia wa pande
zote mbili. Nyuso hizi zinaonesha furaha ilivyotawala sherehe hiyo Mr and Mrs Reginald Mengi wakiwa na nyuso za furaha pamoja na watu wao wa karibu Ndoa
hiyo imefungwa ikiwa ni miezi minne tu baada ya Mengi kumchumbia rasmi
Jacky kwenye sherehe ya siku yake ya kuzaliwa (K-Lynn) iliyofanyika
December mwaka jana mjini Dubai. Dr.
Mengi na mke wake Jacqueline wakiwa wamewashika mikono watoto wao
mapacha wakati wakitembea kwenye moja ya fukwe za bahari ya Hindi nchini
Mauritius ilikofungwa ndoa yao Kwa mujibu wa watu wao wa karibu waliohudhuria, sherehe hiyo ilitawaliwa na furaha ya hali ya juu. Dr. Reginald Mengi akimsaidia mke wake Jacqueline kukata keki ya harusi Bibi harusi, Jacqueline na marafiki zake wa karibu wakiwa kwenye furaha kubwa baada ya kiapo cha wanandoa Congratulations to the newlyweds!