MAREALLE APEWA TENA UKAMANDA WA VIJANA WA CCM

Admin Updates11 years ago3 Views


 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka Wilaya ya Moshi Mjini(MNEC) Kamanda wa vijana UVCCM Bw Agrey Marealle Akila kiapo cha utii kwa CCM wakati wa kusimkwa kuwa Kamanda wa vijana wa CCM wilayani humo mbele ya mgeni rasimi Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mboni Mhita(hayuko pichani)



 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka Wilaya ya Moshi Mjini(MNEC) Bw Agrey Marealle akiwa amekalishwa kwenye kigoda huku akiwa na ngao na mkuki mara baada ya kusimikwa kuwa Kamanda wa vijana UVCCM wilayani humo na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mboni Mhita(hayuko pichani)



 Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mboni Mhita(kushoto) akimvalisha kofia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka wilaya ya Moshi Mjini Bw Aggrey Marealle kuwa Kamanda wa Vijana wa CCM wilayani humo Mjini katika halya iliyofanyika viwanja vya CCM katab ya Njoro.


Mkamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mboni Mhita(kushoto) akimkabidhi mkuki Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka wilaya ya Moshi Mjini Bw Aggrey Marealle katika hafla ya kumsimika kuwa Kamanda wa Vijana wa UVCCM wilayani humo katika sherehe ya kumsimika iliyofayika katika viwanja vya CCM kata ya njoromjini humo.


=======  =======  =======


Marealle apewa tena Ukamanda wa Vijana wa CCM Moshi Mjini



*Ahimiza mshikamano kwa wanaCCM




MJUMBE wa halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi, (CCM), kupitia Moshi  Mjini, mkoani Kilimanjaro, Aggrey Marealle, amesema mshikamano   miongoni mwa wanachama wa chama hicho ndiyo pekee utakaopelekea chama    hicho kufanya vyema katika chaguzi zijazo.








Bw. Marealle aliyasema hayo juzi mjini Moshi, wakati wa hafla ya

kusimikwa kwake kama kamanda wa vijana wa umoja wa vijana wa CCM,

(UVCCM), wa wilaya ya Moshi Mjini  kwa kipindi cha pili cha miaka

mitano, hafla iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa tawi la wakereketwa

la Marealle lililopo Kata ya Bondeni, Moshi Mjini.




“Changamoto kubwa ambayo CCM imekuwa ikikumbana nayo nyakati za

kuelekea chaguzi mbali mbali ni kutokuwa na mshikamano jambo ambalo

mara nyingi hutokana na makundi ndani ya chama, ni vyema tukaepuka

hili na msamiati wetu mpya uwe ni mshikamano, hapa tutashinda”,

alisema.




Aidha alitoa wito kwa wananchi hususan wanachama wa CCM kutokutumia

changamoto za kimaisha walizonazo kama sehemu ya maamuzi katika 

kuchagua viongozi na mstakabali mwingine wa kisiasa.




Katika hafla ya uzinduzi wa tawi hilo la wakereketwa, Bw. Marealle

alisema kada ya vijana ni nguzo ya Taifa ambayo haina budi kulindwa

kwa kuhakikisha maswala yanayowahusu yanapewa kipaumbele ili wasikate 

tamaa.




Akihutubia katika hafla hiyo ambayo ilienda sanjari na kusimikwa

makamanda wapya wa UVCCM Kata zote za Moshi Mjini, Makamu Mwenyekiti    

wa UVCCM Taifa, Mboni Mhita, alisema kuwa kazi kubwa ya makamanda wa    

vijana wa CCM ni kuwaunganisha vijana, kubaini kero zao na  

kuzishughulikia kwa wakati.




Bi Mhita alielezea kazi zingine kuwa ni pamoja na kuwasaidia vijana

kupata ajira za zikiwemo zile za kujiajiri wenyewe pamoja na kutoa

ushauri kwa vijana unaohusiana na mwelekeo wa kisiasa na kimaisha kwa

ujumla.




“Kwa kufanya hivi mtakuwa mnaweka nguzo imara ya Taifa kwa ajili ya

miaka mingi ijayo”, alisema na kutoa wito kwa vijana kuwa tayari

kupokea ushauri watakaopata kutoka kwa makamanda hao wapya wa vijana.




Aidha aliwaasa vijana kuiepusha na matumizi ya dawa za kulevya pamoja

na anasa zilizopitiliza ambapo alisema mambo hayo yanachangia kwa


kiasi kikubwa kupunguza ari na nguvu kazi ya Taifa.

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.