Nimekuwa kwenye uhusiano na mpenzi wa roho yangu kwa takriban miaka mitatu.
Kwa kipindi chote hicho tumekuwa tukiishi mikoa tofauti. Yeye anafanya kazi Babati na mimi nafanya kazi Dodoma.
Licha
ya umbali uliopo tumeishi kwa upendo na kuaminiana na hata ndugu na
wazazi wanajua kuhusu uhusiano wetu tukitarajia kuja kufunga ndoa
baadae.
Siku
za karibuni amekuwa akisisitiza sana nikatoe mahali kwao nami nikawa
namuambia sawa tutafanya hivyo na nimemueleza sababu ya kuchelewa ni
matatizo ya kifamilia yanayonikabili.
Ghafla wiki iliyopita alikata mawasiliano na hataki pokea simu yangu wala kujibu sms.
jana
nimekaa nawaza akanitumia sms kuwa nadhani nishaamua kama namhitaji
niende kwao Marangu kabla ya tar 29 mwezi huu vinginevyo simuhitaji.
Kweli
nimeishiwa nguvu kwa kuwa sidhani kama kwenda kwao kwa kuforce kwa
deadline ni vyema. Anajua kuwa nampenda sana lakini sasa hakuna my love
wala sweet.. Ni mwendo wa hey na hello yan full ubabe. Nishaurini wakuu
maana natarajia kwenda lakini kwa sasa sijajipanga kusema kweli