Akizungumza kwenye The Sporah Show, Lulu amezitaja sababu za kupendelea kutoka na wanaume waliomzidi umri.
SPORAH: Watu wanahisi kwamba Lulu anapenda sana kutembea na watu waliomzidi umri sana,
LULU: That’s true, sio uongo, sio sana, Napenda kudate mtu ambaye
anayeweza kusimama kama mpenzi, kama kaka, kama baba, kama kiongozi.
Sitakuwa tayari kuwa na ile relation leo tumeamka na Maisha Club, kesho
tumeamka na Billicanas, kesho tumeamka pale tunakula chips, I need to
gain from you, nje ya upenzi unanifundisha nini kwa sababu haimaanishi
kwamba mi ntaishi na wewe milele, itafikia siku labda we utaondoka au mi
ntaondoka, we ukiondoka mi nikibaki nimejifunza nini kutoka kwako na
ntaendelea kuishi vipi.”
“Haimaanishi kwamba napenda kutembea na watu walionizidi umri labda
miaka hamsini, napenda kuwa na mtu ambaye angalau ananizidi umri,
anauzoefu zaidi yangu, amepitia vitu vingi, anajua vitu vingi kwamba
i’ll be there as a girlfriend lakini nakuwa naiba iba kidogo […] na vitu
vingine vya kitoto kitoto vingi vinakuwa hamna.” alisema Lulu.
Bongo 5