KITUKO:HEBU ONA HAWA WAREMBO WA CHINA WASHINDANA KUTUPIA PICHA MTANDAONI WAKIONYESHA NYWELE ZAO ZA MAKWAPANI

10 years ago127 Views

KATIKA hali ya kushangaza mastaa mbalimbali na warembo  nchini China wameamua kutupia picha zao mitandaoni wakionyesha nywele zao za makwapani katika kushiriki shindano la picha za kwapani kwa wanawake.

Mwanzilishi wa shindano hilo, Xiao Yue anasema uzuri wa mwanamke si lazima asiwe na nywele kwapani na kuongeza kuwa shindano hilo halimaanishi kuwa wanawake wasinyoe nywele hizo ila nia yake ni kuondoa dhana potofu kuwa nywele hizo hazikubaliki kwa mwanamke na kuonekana jambo la aibu kwa wenye tabia ya kuziacha..

Mshindi wa shindano hilo atakayekuwa ametokelezea na kujiamini atapata zawadi nono katika shindano hilo lililoanza Mei 26, mwaka huu.

Mtandao wa Weibo umejaa picha za warembo mbalimbali walioshiriki shindano hilo litakalomalizika Juni 26, mwaka huu wakiwa na furaha kuinua mikono yao juu na kuonyesha makwapa yao yenye nywele kwa dunia nzima.


Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.