KIGOGO WA MADINI AMFANYIA PATI MDADA KELVINA WA BONGO MUVI..CHEKI HII PATI HAPA

Admin Updates9 years ago8 Views

Msanii wa filamu Bongo, Kelvina John na kigogo mmoja wa migodini Bulyanhulu, Injinia Paulo Maira.
Hamida Hassan, Gladness Mallya
Msanii wa filamu Bongo, Kelvina John juzikati alifanyiwa bonge la pati na kigogo mmoja wa migodini Bulyanhulu, Injinia Paulo Maira ambaye alimmwagia ‘mapesa’ na kumuahidi ndoa ‘soon’ baada ya kumtolea mahari.
Kelvina akihesabu pesa alizozawadiwa na kigogo huyo.

Pati hiyo ilifanywa maalum kwa ajili ya kumpongeza kwa kutimiza miaka 32 ya kuzaliwa ambapo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Jozi Lounge ‘Msasani Village’, Msasani jijini Dar.

Injinia Paulo akimzawadia pesa Kelvina

Akizungumza kwa furaha kwenye pati hiyo, Kelvina alimshukuru Mungu kupata mwanaume anayempenda ambaye amembadili kutoka kwenye maisha f’lani na kuelekea kwenye ndoa.

 Kelvina akionesha pesa alizozawadiwa

“Mtarajie ndoa hivi karibuni kwani nimeshatolewa mahari jamani, nimeamua kuolewa na wala sitarudi nyuma, unajua mtu kukukubali ukiwa tayari na watoto wawili kwangu naona ni upendo wa hali ya juu,” alisema Kelvina kwenye pati hiyo iliyohudhuriwa na mastaa kibao.

Sherehe ikiendelea.

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...