JANUARI MAKAMBA, BILIONEA MENGI NA PROF. MUHONGO WANG’ARA…

Admin Updates10 years ago3 Views

Naibu
Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano, Januari Makamba pichani
juu ametajwa kuwa mwanasiasa bora kijana na taasisi ya Tanzania Awards
International, jijini Dar es Salaam juzi.
Makamba
ameshika nafasi hiyo akiwapita wanasiasa wengine vijana ambao ni pamoja
na Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, Katibu wa Itikadi
na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John
Mnyika, Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, Wabunge Vick Kamata,
Esther Bulaya, David Kafulila na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Mboni Mhita.
Katika
tuzo za mwanasiasa mtu mzima ushindi umechukuliwa na aliyekuwa Waziri wa
Nishati na katika kundi hilo, Profesa Muhongo alishindanishwa na Waziri
Mkuu Mizengo Pinda, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, Waziri
Sheria na Katiba, Dk. Asha Rose Migiro na Waziri wa Nchi Katika Ofisi ya
Makamu wa Rais, Muungano, Samia Suluhu.

Wengine
ni Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, Waziri wa Ujenzi Dk. John
Magufuli, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison
Mwakyembe, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira na
Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Liberata Mulamula.

Tuzo ya jamii ilichukuliwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi.
Waliopewa
tuzo za heshima katika jamii ni Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere
na Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Hayati Nelson Mandela.

Si Makamba, Profesa Muhongo wala Mengi waliohudhuria shughuli hiyo badala yake waliwakilishwa na ndugu zao.
Hata
hivyo sherehe za kutoa tuzo hizo zilidororora hasa kwa kuwa Rais Jakaya
Kikwete aliyepangwa kuwa mgeni rasmi hakuhudhuria na aliwakilishwa na
mkuu wa mkoa lakini naye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala,
Raymond Mushi.

Akitoa
ufafanuzi wa tuzo hizo, Mratibu wa Taasisi hiyo, Amani Mwaipaja alisema
zilikuwa katika vipengele vitano ambavyo ni tuzo ya jamii 2015, tuzo za
jamii ya heshima, tuzo jamii katika haki za binadamu, tuzo ya mwanasiasa
kijana na tuzo ya mwanasiasa mzee.
“Tumeangalia
vigezo kadhaa ikiwa pamoja na uadilidu, uaminifu, utii katika sheria,
kuwa na maono, mikakati na mipango,” alisema Mwaipaja.
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.