Katibu Mkuu, Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, pamoja na wataalamu wengine wa Serikali, leo wamehudhuria Mkutano Unaoendelea wa 45 wa Kamati ya Urithi wa Dunia ya UNESCO jijini Riyadhi, Saudi Arabia, ambapo pamoja na mambo mengine Tanzania itasisitiza juu kuendelea kuenziwa kwa vivutio vyetu mbalimbali vilivyomo kwenye orodha ya Urithi wa Dunia ili kuendelea kuvuta watalii wengi zaidi kutoka mataifa mbalimbali kuja nchini. Vivutio saba vya kiutamaduni (cultural) na asili (natural) vya Tanzania ambavyo vipo kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia na mwaka wa kuingizwa orodhani ukiwa kwenye mabano ni:
1. Hifadhi ya Serengeti (1981);
2. Jiopaki ya Ngorongoro (1979);
3. Pori la Akiba la Selous (1982);
4. Mji Mkongwe wa Zanzibar (2000)
5. Michoro ya Mapangoni Kondoa (2006);
6. Magofu ya Kilwa Kisiwani na Kisiwa cha Songo Mnara (1981); na
7. Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (1987).