DK. BASHIRU AWATAKA CCM WASIFANYE UHUNI HUU

Special Correspondent6 years ago7 Views

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally, amewataka wanachama wa CCM kuheshimu alama za vyama vyote vya siasa nchini kwa sababu vimesajiliwa kisheria.

Dk Bashiru amesema hayo wakati akizindua mkakati wa kukomaza demokrasia kwenye mashina ulioandaliwa na CCM mkoa wa Dodoma.

Amewataka kutochoma wala kubeza alama za vyama hivyo na kwamba huku akigusia suala la wafuasi wengine kuchoma bendera na kupaka rangi ya chama chao ofisi za chama kingine.

“CCM tusifanye mambo holela na uhuni huo katika siasa. Ni kosa kuparamia na kupaka rangi ofisi za vyama hivyo. CCM tusifanye hivyo ni kosa kisheria”. amesema.

Ameongeza, Sisi wanachama wa Chama cha Mapinduzi tunao wajibu wa kulinda uhuru wa vyama vingine vilivyosajiliwa kisheria, kama sisi tunafurahi na kuimba nyimbo zetu acheni na wao wafurahi na kuimba nyimbo zao, kama sisi tunapendeza na nguo zetu acheni na wao wapendeze na nguo zao.

Chanzo – EATV

from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/2U8M62G
via

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Previous Post

Next Post

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...