Kwa muda mrefu, Diamond Platnumz alikuwa akilijua tatizo la mpenzi wake wa zamani Wema Sepetu la kutoshika mimba.
Akiongea
na kipindi cha Ng’ari Ng’ari cha Clouds TV, Diamond alisema wakati wako
pamoja waliwahi kuzunguka kwa wataalam mbalimbali kujaribu kupata tiba
lakini hawakufanikiwa.
Alisema ilifika wakati alimweleza tu kuwa akubali hali hiyo.
Kuhusu
kile Wema alichokiandika kwenye Instagram hivi karibuni ambapo alieleza
ukweli wa hali yake ya kutopata mtoto, Diamond alisema ujumbe huo
ulimuumiza kama wengine walivyoumia.
Alisema alikuwa anafahamu jinsi
watu wanavyomshambulia Wema kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kutopata
mtoto na amemsifia kwa kuusema ukweli.
Hata hivyo aliwashauri
watumiaji wa mtandao ya kijamii kuitumia vyema na sio kuitumia kuwatusi
mastaa wao kwakuwa ni kweli maneno yao huwaumiza kama binadamu wengine.