Bundi Azua Taharuki Bungeni….Spika Awatoa Hofu Wabunge

Special Correspondent6 years ago8 Views

Bundi Azua Taharuki Bungeni....Spika Awatoa Hofu Wabunge

Katika hali isyo ya kawaida Ndege aina ya bundi ameonekana Bungeni akiwa juu kabisa.

Spika wa bunge, Job Ndugai, amemshuhudia Bunge huyo laivu na kusema alipomuona alichanganyikiwa kidogo na kisha akawatoa hofu Wabunge kuwa kwa Dodoma kumuona ndege huyo mchana si tatizo isipokuwa ukimuona usiku ndio unaweza kuogopa.

Watumishi wa Bunge waliingia ndani ya jengo hilo kwa ajili ya ukaguzi na kumuona ndege huyo juu ya paa la ukumbi wa Bunge.

Ndege huyu hakutoka licha ya maofisa hao kutaka kumtoa, aliruka kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Hata hivyo, haikujulikana  muda aliotoka na mahali alikoelekea lakini Spika Job Ndugai akasema ni mambo ya kawaida kwa Dodoma.

“Waheshimiwa wabunge, asubuhi tumeanza kumwona Bundi ndani ya jengo hili, lakini kwa Dodoma Bundi wa mchana hana madhara kwa hiyo ni mambo ya kawaida kabisa,” amesema Ndugai.

from UDAKU SPECIAL BLOG http://bit.ly/2HCUfHO
via

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...