Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo ametaja orodha ya watu mbalimbali wanaojihusisha na dawa za kulevya jijini Dar es Salaam na kusema kuwa yupo tayari kwa ajili ya mapambano dhidi yao.
RC Makonda alisema kuwa yupo tayari kuuupoteza ukuu wake wa mkoa na hata kupoteza uhai wake lakini akifika mbele za Mungu apate kitu cha kusema kuwa alipewa nafasi na akatumia kupambana na janga hili linalohatarisha nguvu kazi ya taifa.
Katika orodha iliyotolewa na RC Makonda, wamo watu wa makundi mbalimbali ambapo kuna wanaouza dawa za kulevya, wanaosambaza na wanaotumia dawa hizo.
Katika watu hao kuna wasanii wa muziki nchini Tanzania, watu maarufu na maafisa wa Jeshi la Polisi ambao wamedaiwa kuwa wanakwamisha upelelezi juu ya kesi hizi
Miongoni mwa wanii waliotuhumiwa kutumia dawa za kulevya ni pamoja na Wema Sepetu, Rachel, Babu wa Kitaa, Mr. Blue, Chid Benz na wengine. Hapa chini ni video ya RC Makonda akizungumza na waandishi wa habari mapema leo;
WhatsApp Image 2017-02-02 at 1.07.35 PMWhatsApp Image 2017-02-02 at 1.07.35 PM (1)