
Biashara zisizoruhusiwa kufanywa na Raia wa Kigeni Nchini Tanzania.
Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt.Samia Suluhu Hassan kushangazwa na baadhi ya watendaji wa Serikali kutoa leseni za biashara ndogo ndogo kwa wageni huku akitolea mfano Mchina muuza Mitumba Kariakoo ambapo alimwagiza Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemean Jaffo kutafuta ufumbuzi wa jambo hilo mara moja.
Rais Samia lisema baadhi ya wageni Wamefika mbali saa hizi wamejigeuza Wachimbaji Wadogo wa Madini naelekeza Hii tabia ikomeshwe mara Moja kwa Wizara zinazohusika.
Baada ya Rais Samia Suluhu kutoa maelekezo hayo muhimu, Dkt. Selemani Jafo kuangalia suala la raia wa kigeni kupewa leseni za kufanya biashara zinazofaa kufanywa na wenyeji,Waziri jafo alichukua hatua stahiki kwa kuhakikisha anapokea maoni ya kamati ya wafanyabiashara wa Soko la karikoo ambapo amehakikisha Wizara yake imepitisha kanuni na kupitishwa na Bunge zilizoweka wazi aina za biashara zisizoruhusiwa kufanywa na wageni nchini Tanzania kwani hizo ni aina ya biashara ambazo zinatakiwa kufanywa na raia wazawa tu.
SOMA AINA YA BIASHARA ZISIZORUHUSIWA KUFANYWA NA WAGENI ZILIZOPITISHWA NA BUNGE NA KUSAINIWA NA WAZIRI SELEMANI JAFFO







