Mnenguaji wa Kundi la Kanga Moko, Zawia Hamis
Semhando na Zawia ambao ni mastaa wa kundi maarufu la minenguo Khanga
Moja (ambao majuzi walipata msukosuko wa kufyatuliwa risasi mtaani),
wamepata lebo na studio ya Fire Music ya jijini Dar es Salaam na kupakua
wimbo unaokwenda kwa jina la “Ayaya” ambao utawatambulisha katika
ulimwengu mwingine wa sanaa – ulimwengu wa uimbaji.
mtendaji wa Fire Music, Masoud Kandoro, ameiambia Saluti5 kuwa wimbo
huo upo katika hatua za mwisho na kwamba wakali hao ambao
watajitambulisha kama WADADA WAWILI wameutendea haki wimbo huo.
“Ni
wimbo mkali, Wadada Wawili wameimba vizuri na kilichobakia ni mambo
madogo madogo, tunataraji kupata rap fupi fupi za Msafiri Diuof ili
kuunogesha zaidi,” alisema Kandoro.
Wimbo
huo umetungwa na kupangiliwa sauti na H- Mbizo ambako ndani yake
utakutana na mistari kama “Penye miti hakutaki wajenzi, panataka
wakwezi”, “Dukani kumejaa vipodozi kuzaa kunataka malezi”, “Taarab
haionogi mapozi inanoga mashauzi”.
H- Mbizo ndiye aliyetunga wimbo wa “Majanga” uliompatika sifa kibao mwanadada Snura.
