Usiku
wa kuamkia leo ulikuwa ni usiku wa furaha kwa staa wa Filamu Bongo,
Rose Ndauka, kwani aliweza kusheherekea siku yake ya kuzaliwa na baadhi
ya mastaa wenzake waliyofurika ndani ya Hoteli ya Collossium iliyopo
maeneo ya Kamata Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Rose
Ndauka (kushoto), akimlisha kipande cha keki rafiki yake mpendwa Jack
Pentzel, muda mfupi baada ya zoezi la kulishana keki kuanza kwenye
sherehe yake ya kuzaliwa iliyofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya
Ukumbi wa Collosseum Hoteli Kamata Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.