Angalia hapa Mbunge Abdallah Chikota alichofanya Jimboni kwake Nanyamba jana

Admin Updates10 months ago6 Views

  

Mbunge wa Jimbo la Nanyamba Mhe Abdalla Dadi Chikota 
 tarehe 14/7/2024 amefanya ziara yake kwa siku ya pili kata ya Kitaya katika vijiji vya Mayembe Juu, Mchanje, Kitaya na Kihamba.

Katika Ziara hiyo Mhe Chikota amechangia mifuko ya saruji Kijiji Cha Mayembe Juu mifuko 100, Mchanje mifuko 100 Ofisi ya Kijiji Cha Kitaya Bati 40 kutokana na ahadi yake ya kuchangia maendeleo yaliyoanzishwa na wananchi wenyewe kama vile ujenzi wa zahanati.

Akitoa vifaa hivyo vya Ujenzi Mhe Chikota pia ametoa fedha taslimu millioni Moja kwa Ndg Mahafudh Hassani Chitimbe wa Kijiji Cha Dindwa.


Ndg Chitimbe amemshukuru mbunge kwa kumpatia fedha hiyo kama ahadi yake aliyoomba ili aendeleze Kilimo chake Cha umwagiliaji.
Nae Mwenyekiti wa CCM Mtwara Vijijini katika Ziara hiyo amewasisitiza wananchi wa kata ya Kitaya kujitokeza kwenye zoezi la Uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura mara baada ya zoezi hilo litakapoanza ili wenye Sifa wote waweze kupiga kura katika Uchaguzi wa serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.