Msaidizi wa Kazi za Nyumbani Amshtaki Bosi Wake Kwa Kutomlipa Mshahara Kwa Miaka Mitano

Admin Updates2 years ago6 Views

 

Zuhura Ramadhani (30) amemshtaki Khadija Katusi Muoza katika Serikali ya Mtaa ya Mpiji Magohe kwa kutomlipa stahiki zake kwa zaidi ya Miaka mitano ambapo kwa mwezi mshahara wake ni Tsh. 35,000
Zuhura anasema “Nimefanya kazi kwake kwa Miaka 14 kwa wema, nimewalea Watoto wake vizuri, ilifikia kipindi nilikuwa natoa Fedha zangu kusaidia Familia yake. Alisema mambo yake si mazuri na ananihifadhia Mishahara yangu, Mama yangu anaumwa na ninahitaji kumuuguza”
Upande wa Khadija amesema “Kweli ananidai, nimeishi naye vizuri na kuna muda alikuwa akitoa Fedha zake kusaidia Familia lakini Maisha yameyumba, nikipata Hela nitamlipa.”
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, Saidi Diuchile amesema “Khadija amekubali kwa maandishi kuwa atalipa lakini kumekuwa na ugumu kutekeleza, baada ya mvutano amelipa Tsh. 200,000 kati ya zaidi ya Tsh. 2,860,000 ambayo anadaiwa.”
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...