MPYA:Papa Francis Amtimua Askofu Anayepinga Mabadiliko

Admin Updates1 year ago6 Views

Papa Francis amemfuta kazi askofu Joseph Strickland, ambaye ni mkosoaji mkubwa ambaye ameibua maswali juu ya uongozi wa Papa katika Kanisa Katoliki.

Kwa mujibu wa taarifa ya Vatican, askofu huyo ameondolewa madarakani kufuatia uchunguzi katika Dayosisi ya Tyler, huko Texas, Marekani aliyokuwa akiiongoza.

Askofu Strickland ni mmoja kati sauti kinara katika tawi la uongozi wa Kanisa Katoliki nchini Marekani ambalo linapinga vikali mabadiliko yanayopigiwa chapuo na Papa.

Kuondolewa kwake kunakuja baada ya Papa kuzungumzia juu ya hali “ya kuwa nyuma” kifikra ya baadhi ya viongozi wa Kikatoliki nchini Marekani.

Askofu Strickland mara kadhaa ameshambulia hatua za Papa kutaka kubadili msimamo wa Ukatoliki katika masuala kadhaa ya kijamii ikiwemo kutoa mimba, haki za waliobadili jinsia na ndoa za jinsi moja.

Mwezi Julai mwaka huu, alionya kuwa mafunzo mengi ya Ukatoliki ambayo ni ya “ukweli wa msingi” yalikuwa yanapingwa, ikiwemo kile alichokiita majaribio ya “kudunisha” ndoa “kama ilivyoundwa na Mungu” baina ya mwanamume na mwanamke tu.

Askofu huyo pia amekosoa majaribio hayo aliyoyaita ya “kuvunja miiko” na kusema wanaoyapigia chapuo “wanapinga utambulisho wao wa kibailojia waliopewa na Mungu”.

Katika barua yake ya mwezi Julai, askofu Strickland amedai kuwa majaribio “kubadilisha visivyobadilika” yatasababisha mfarakano mkubwa ndani ya Kanisa. Na wale wanaotaka mabadiliko, ameonya kuwa “ndio hasa wanaofarakanisha [Kanisa]”.

Askofu Strickland alikuwa chini ya uchunguzi wa Vatican na hapo awali alitupilia mbali uwezekano wa kujiuzulu, na katika barua ya wazi mwezi Septemba alimtaka Papa amfute kazi.

“Siwezi kujiuzulu kama Askofu wa Tyler kwa sababu kufanya hivyo itakuwa ninawatelekeza wana kondoo,” alisema.

Tunaendelea kukupa maelezo zaidi kuhusu taarifa hii.

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.