KUNDI la watu wanaodhaniwa ni majambazi, wamevamia na kupora fedha
taslimu na vitu mbalimbali katika Kanisa Katoliki la Kilema, Jimbo la
Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Desemba 14, mwaka huu, ambapo watu
hao wakiwa na vifaa maalumu vya kuvunja milango, walivunja lango kuu la
kanisa hilo, kuvunja sanduku la sadaka na kupora vifaa vya kufanyia
ibada.
Kanisa hilo ni la kwanza kujengwa na Wamisionari wa kwanza Kanda ya
Kaskazini, inayojumuisha mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Dodoma.
Akizungumza kwa njia ya simu jana, Padri wa Parokia ya Kilema, Damien
Temere Mosha, alisema vitu vilivyoibwa ni pamoja na vifaa vitakatifu
vinavyotumika katika sikukuu ya Ekaristi.
Akizungumza na gazeti hili, Paroko wa Parokia ya Kilema, Padri Mosha
alisema majambazi hao walivunja kasha la kuhifadhi sadaka na kupora
fedha zilizokuwamo, ambazo hazijajulikana thamani yake.
Alisema majambazi hao waliiba vifaa vya kunywea divai na komunio,
ambavyo ni vya dhahabu. Padri Mosha alisema majambazi hao walivunja
kasha maalumu la kuhifadhi vifaa vya ibada na kuiba vile vya dhahabu tu
vyenye thamani ya mamilioni ya fedha huku wakiacha vya shaba.
Alisema baadhi ya vifaa hivyo vilinunuliwa na wamisionari wa kwanza na
vilikuwa na thamani kubwa kwa Kanisa hilo, kwa kuwa viliwakilisha imani
katika parokia hiyo na Kanda nzima ya Kaskazini.
Kiongozi huyo wa kanisa alibainisha kuwa jambo lililomsikitisha ni namna
eneo takatifu la kanisa hilo lilivyoharibiwa vibaya, kwani eneo hilo
mara nyingi limekuwa likitumika kwa ajili ya kutolea sakramenti takatifu
kwa mujibu wa utamaduni wa Kanisa hilo Katoliki.
Aliwataka wakazi wa Kilema na wanaozunguka eneo hilo kuwa na utulivu
wakati huu vyombo vya usalama vikiendelea na uchunguzi hadi pale
waliohusika na tukio hilo watakapokamatwa na kuchukuliwa hatua.
Waumini wa kanisa hilo ambao walikusanyika kwa ajili ya sala yao ya
kawaida ya Jumapili majira ya saa moja asubuhi, walijikuta wakichelewa
kuanza misa wakati uongozi wa kanisa hilo, ukijaribu kutengeneza na
kusafisha maeneo yote yaliyoharibiwa na majambazi hao.
Nje ya mlango wa kuingilia kutoa sadaka, kulikuwa na damu na inasadikiwa
kuwa huenda ni za mmoja wa watu hao waliovamia kanisa hilo alijeruhiwa
wakati akijaribu kuvunja mlango huo, ambao hufungwa kwa vitasa imara.
Mosha alisema katika tukio hilo, hakuna mtu aliyejeruhiwa au kupoteza
maisha. Paroko huyo alitangaza kuwa kanisa litatoa zawadi ya Sh milioni
mbili kwa mwananchi yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa majambazi hao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Geofrey Kamwela alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo. Alisema taarifa rasmi itatolewa baada ya
uchunguzi kukamilika.
Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win