MWIZI WA GAUNI LA LUPITA NYONG’O ALIRUDISHA BAADA YA KUGUNDUA NI FEKI NA HALINA THAMANI YA $150,000

Admin Updates10 years ago7 Views



Mwizi aliyeiba gauni la muigizaji Lupita Nyong’o alilovaa kwenye tuzo za
2015 Oscars ameamua kulirudisha baada ya kugundua kuwa ni feki na
halina thamani iliyotajwa.

Gauni hilo la Calvin Klein lililotengenezwa maalum kwaajili ya Lupita,
lilimvutia mwizi huyo kulinyemelea na kuliiba baada ya kudaiwa kuwa na
thamani ya $150,000 (zaidi ya shilingi milioni 274).

Mwizi huyo aliwapigia simu mtandao wa TMZ na kuwaelekeza alipoliacha
begi lenye gauni hilo, na TMZ walitoa taarifa polisi ambao walilifatilia
na kulikuta limerudishwa hotelini lilipoibiwa lakini likiwa limewekwa
bafuni chini ya sinki.

Mtu huyo aliiambia TMZ kuwa aliliiba gauni hilo kwenye chumba cha Lupita
baada ya kukuta mlango ukiwa wazi, na kubandua vigolori viwili na
kuvipeleka kwa wataalam wambao walimwambia ni za bandia.

Mwizi huyo aliongeza kuwa aliamua kurudisha gauni hilo na kuwapigia simu
TMZ ili kuumbua uongo wa mastaa wa Hollywood, na ulimwengu ujue kuwa
gauni hilo halina thamani iliyotajwa.

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...