ROSE NDAUKA & MALICK BANDAWE
Rose anayefanya vizuri katika gemu la filamu Bongo na Malick
walimwagana wakiwa katika hatua za mwisho za kuingia kwenye ndoa kwani
ndiyo vikao vya harusi vilikuwa vianze.
Rose aliishia kuzalishwa na Malick na uchumba wao ukavunjika kwa kile
kilichodaiwa ni kukosekana kwa uaminifu ambapo hadi sasa kila mmoja ana
maisha yake.Mashabiki waliipenda kapo hiyo kwani Rose baada ya kuwa na
Malick alibadilika hivyo mabadiliko yake yakawa yanawavutia baadhi ya
watu.
RAY & MAINDA
Uhusiano wa mastaa hao wa filamu za Kibongo
ulitikisa enzi hizo na ulidumu kwa muda mrefu japokuwa walikuwa
wakifanya siri lakini baada ya kuachana Mainda aliweka wazi jinsi yeye
na Ray walivyochezeana na kuachana.
Mainda na Ray waliachana baada ya Ray kuwa na uhusiano wa kimapenzi
na msanii mwenzake, Chuchu Hans ambapo baada ya kumwagana kwa wawili hao
mashabiki wengi walilalamika na hadi leo wanatamani Mainda na Ray
warudiane kwani walikuwa wanaendana tofauti na Chuchu Hans lakini ndiyo
hivyo wameachana njia panda.
AMANDA & BWANA MISOSI
Amanda aliingia kwenye mahaba mazito
na Bwana Misosi ambapo alimtambulisha hadi kwa ndugu huku wakitangaza
kwamba lazima waoane lakini mbio zao ziligonga mwamba baada ya
kumwagana.
Kwa sasa wawili hao wamebaki stori tu japokuwa hakuna
ambaye yupo tayari kufunguka sababu za kuachana kwao lakini kila mmoja
anaendelea na maisha yake mengine.
AUNTY LULU & BOND
Uhusiano wa mastaa hao ulidumu kwa muda
mrefu japokuwa ulikuwa ni wa kupigana mangumi kila wakati lakini
walikuwa wakipendana. Wawili hao walikuja kumwagana na kila mmoja
kuchukua hamsini zake.
Kwa sasa Bond anadaiwa kuwa kwenye uhusiano na mwigizaji mwenzake, Wastara Juma huku Aunty Lulu naye akiwa na uhusiano mwingine.