- Home
-
- STAA NEY WA MITEGO AMKANA MPENZI WAKE (SIWEMA)..KISA NI HIKI HAPA
STAA NEY WA MITEGO AMKANA MPENZI WAKE (SIWEMA)..KISA NI HIKI HAPA

Msaniii
Emmanuel Elibarick alimaarufu kama Mr Nay ameonesha dalili ya wazi kuwa
hana mpango tena wa kuwa katika mahusiano na Mchumba wake huyo Siwema
ambaye amezaa nae mtoto wa kiume aitwae Curtis miezi kadhaa
iliyopita.Kupitia ukurasa wake wa Instgram Nay wa mitego siku mbili
zilizopita aliweka post ambayo ilikuwa inasema kuwa kwa sasa ana watoto
watatu na ana mapenzi ya kweli na watoto wake lakini hana mpango wala
hana mahusiano ya kimapenzi na mama wa watoto wake hao bali anawaheshimu
wanawake hao kama wazazi wenzake.
“Mr_Nay Baba
wa watoto watatu… Sina Mke I mean Sijaoa na sina mahusiano ya
kimapenzi na Mwanamke yoyote Yule… Kati ya niliozaa nao. Nawapenda
watoto wangu nawaheshim mama zao..SingleBoy am in love with my son and
daughters… Rishma, Curtis na Munie”
Kwa upande wake Siwema ambaye
ni mama wa Mtoto wa Nay juzi aliweka picha ya Mzazi mwenzake na kuwataka
mashabiki zake wafunguke lolote juu ya picha ile ila Comment nyingi
zilionesha kuwa watu hao hawapo sawa au hawapo pamoja kwa sasa kama
ambavyo baadhi zinasema.
“kaysamira: Siwema Mimi nakupenda siwez
kukujudge chochote sababu mapenzi upofu namuomba Mungu akupe jicho la
tatu na uweze kusonga mbele,mambo kama hayo hutokea na yanapita na kama
yeye hakutaki usijali kuna wanaume wengi tu wanaopenda kuwa na mtu kama
wewe tena wazuri kuliko yeye labda ndio chance mungu kawapa ili uweze
kukutana na prince charm wako lakini kama umeandikiwa kuwa na baba
Curtis hakuna mwenye kupinga hilo lakini aache kuwadhalilisha na kutumia
udhaifu wenu kama mwanamke inauma anachezea sana hisia zenu”
“Augustinasimon37:
Hakuna wa kumjudge mtu hapa, mapenzi ni ya wawili tu. kabla hakuzaa
walikuwa sawa wakipendana iweje sasa ndio maana tunaumia, tunawaombea
wasiachane, kibinadam sio vizuri. Nakupenda bure Siwema mpende mtoto
wako ndio kila kitu kwako”
Lakini pia Nay wa Mitego leo amepost picha
akitoka Mwanza huku akiwa na Mwanae Curtis akimnywesha Maziwa ya kopo
hali ambayo inaonyesha wazi kuwa huenda mtoto huyo yupo chini ya himaya
ya baba na si mama tena kitu ambacho kinaweza kutoa majibu ya wazi kuwa
watu hao huenda wameachan
0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)
Stay Informed With the Latest & Most Important News