- Home
-
- BREAKING NEWS: BAADA YA SIKU 96 MBOWE, MATIKU WARUDI URAIANI
BREAKING NEWS: BAADA YA SIKU 96 MBOWE, MATIKU WARUDI URAIANI
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetengua maamuzi ya kufutiwa dhamana yaliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuamuru warufani hao (Mbowe na Matiko) waachiwe huru mara moja.
Aidha imeondoa baadhi ya masharti ya dhamana ikiwemo kuripoti kila wiki kwa Kamishina wa Polisi Mkoa na badala yake wametakiwa kuripoti kila mwisho wa mwezi Kisutu.
Pia imewaamuru washitakiwa kutokusafiri nje ya Tanzania bila kibali cha mahakama na kwamba masharti mengine yaliyokuwepo Kisutu yataendelea kubaki kama ilivyo.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2IYSs0d
via
0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)
Stay Informed With the Latest & Most Important News