ZARI AFUNGUKA KUHUSU UVUMI KUWA HANA MAELEWANO NA BABA WA WATOTO WAKE
Zarinah
“The Boss Lady” Tlale a.k.a mama kijacho au kama anavyofahamika kwa
kifupi Zari, amekanusha uvumi ulioenea kuwa yeye na mme wake wa zamani
ambaye ni baba wa watoto wake watatu, Ivan Ssemwanga kwa sasa
hawazungumzi kutokana na kuwa kwenye mtafaruku mkubwa.
“Nina watoto
watatu wa kiume wa kwanza ana miaka 12 wa pili 10 na mwingine ana miaka 8
wako poa na nina jivunia kuwa mama.” Alisema Zari kupitia E-Newz ya
EATV.
(Kuhusu
baba wa wanaye watatu) “Hatuko pamoja lakini tuko poa kwasababu kuna
vitu vingine vinaendelea kati yetu wakiwemo watoto na mambo mengine
mengi kwahiyo tuko poa. Unajua jinsi watu na vyombo vya habari
wanavyochukulia ni kama tuna ugomvi na hatuzungumzi lakini sisi tuko poa
kabisa.”
Zari pia amezungumzia kuhusu uhusiano wake na Diamond kwa
kusema kuwa mapenzi yao ni ya wao wawili na sio ya watu wengine hivyo
hawapendani ili kuwafurahisha wengine.
“Tuko poa, tunapendana
lakini hakuna info zaidi. Sitaki kutoa taarifa zaidi ambayo tunaita
‘T.M.I’ (Too Much Info) Lazima huwa kuna kuwa na mitazamo hasi na
mitazamo chanya, watu wengine watasema poa wengine watasema sio poa,
lakini mwisho wa siku sio kile watu wanachofikiria na sio kile watu
wanachotaka lakini ni nini sisi tunataka, nini kinachotupa furaha, je
tunafuraha kuwa pamoja tunataka kuwa pamoja, ndo hivyo. Hatudate
kwaajili ya watu, au kwasababu wao wanataka tuwe pamoja.”
0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)
Stay Informed With the Latest & Most Important News