yangu wa damu ninayemfata, ana mchumba wake ambaye wamekuwa pamoja kwa
miaka mitatu sasa, wote ni waajiriwa na wanaishi mikoa tofauti. Mwaka
Jana wakakata shauri waoane, mwanaume kafata hatua zote na vikao
vimeanza.
Miaka iyo yote ya mahusiano, kuna
msichana ambaye huyo bwana alikuwa anatembea naye japo huyo bwana
alikuwa anakana, tena wakati mwingine ananipigia Simu analia nimuombee
msamaha kwa Dada yangu, wanamsingizia sio kweli. Basi na mimi namwamini
nambembeleza Dada yangu wanasameheana mapenzi yanaendelea.
Sasa hiki kipindi cha sikukuu,
akamwambie Dada yangu waende mkoa fulani(sitautaja) wakapumzike sababu
wote wapo likizo. Yule bwana katangulia kule Dada naye kafatia, bwana
kampokea vizuri hadi hotelini.
Kumbe yule bwana pale hotelini kachukua
vyumba viwili( vimefuatana), kimoja kamuweka yule mwanamke ambaye alidai
anasingiziwa, kingine kamuweka mke mtarajiwa( Dada yangu) pasipo wao
kujua.
Mapumziko yakaisha kila mtu akarudi
mkoani kwake, sasa yule mwanamke mwingine kajua ukweli ikabidi amtafute
Dadayangu amwambie ukweli, na mbaya zaidi ana ujauzito wa miezi 4. Huyo
mdada anadai mwanaume alimwambia wameachana na Dada yangu ndiomana yupo
na yeye, na haelewi chochote Kama hata watu wameanza vikao na harusi
ipo
karibuni.
Imebidi amwambie mama mkwe wake, mama
kampigia mwanae lakini bado anakataa sio kweli, hadi picha katumiwa
alizopiga na yule mwanamke anadai zimeeditiwa sio yeye, imebidi mama mtu
ampigie muhusika yaani huyo mdada, huyo mdada kakiri kweli na kweli
mjamzito.
Wazazi wa mwanaume wamesema hawatambui
hilo, binti azae mtoto atachukuliwa, na mipango ya harusi inaendelea,
kachanganyikiwa hajui aamue nini, fahamu zinarudi na kupotea tu.