Watumishi wa TARURA wapatiwa Mafunzo kuhusu Masuala haya Muhimu

Admin Updates5 months ago6 Views

Dodoma

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara  za Vijijini Mhandisi Victor H. Seff ametekeleza ahadi ya kuhakikisha Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kupitia mradi wa RISE imetoa mafunzo maalum kuhusu masuala ya unyanyasaji wa kijinsia na usawa wa jinsia katika utekelezaji wa mradi wa RISE.

Mhandisi Seff kwa kushirikiana na Taasisi za kitaalamu zinazotoa elimu kuhusu kuhakikisha ukatili wa kijinsia unakomeshwa hasa maeneo ya kazi amesema TARURA kama mdau wa maendeleo ya Nchi ni Rai na lengo lao kuona vitendo vya ukatili wa kijinsia havina nafasi kwa jamii kwani TARURA inathamini mchango wa kila mmoja katika kuhakikisha ukatili wa Kijinsia unakomeshwa.

 

Akitoa mada juu ya namna ya kushughulikia masuala hayo nyeti ya ukatili wa kijinsia, Mtoa Mada Bi. Beatrice Mchome amesisitiza katika kushughulikia malalamiko yote yanayopatikana kutoka kwa wananchi kwa usiri na utu wa hali ya juu.

Pamoja na mambo mengine mafunzo hayo yamelenga pia katika kuwajengea uwezo watumishi hao kwa namna bora ya kushughulika na malalamiko hata yanayotokea kati ya mtumishi moja na mwingine kwani kutoshughulikia kunaweza sababisha kupunguza ufanisi wa watumishi hao kwenye mradi.

 Naye, Mratibu wa Mradi wa RISE unaofadhiliwa na Benki ya Dunia, Mhandisi Joel Lwitiko Mwandobo (pichani) kwa niaba ya watumishi  amemshukuru Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff kwa kuwawezesha wawezeshaji na kuhakikisha watumishi wanapatiwa mafunzo hayo muhimu ambapo amesisitiza kwa watumishi hao kufanya kazi kwa bidii na kila mtumishi kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Mafunzo hayo ya siku mbili yamefanyika katika Hoteli ya Midland jijini Dodoma na kuhudhuriwa na wataalam i mbalimbali ambao ni watumishi wa TARURA.

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.