Kwa mujibu wa chanzo makini, wawili hao walianzisha uhusiano wao
mwishoni mwa mwaka jana na sasa mapenzi ndiyo yamekolea hadi kufikia
hatua ya Nay wa Mitego kuanika hisia zake mtandaoni.
“Wamekuwa wakibanjuka kwa siri sana si unajua Nay ana mchumba wake
Siwema, bado hajafanya maamuzi magumu ya kumtosa,” kilisema chanzo
chetu.
Paparazi wetu alifanikiwa kunasa ujumbe wa Nay wa Mitego kwenye mtandao
wa Instagram ambao ulionyesha wakiitana kwa majina ya wapendanao
kuonesha dhahiri wawili hao ni wapenzi.
Mbali na kuitana huko, Nay alionesha kuwa amemmisi Wolper ambapo muda
mchache baadaye naye alijibu kwa kuwa amemmisi pia kisha Nay akaifuta
posti hiyo baada ya kuandamwa na maneno ya wapambe.
lipoulizwa Wolper kama kwa sasa ameamua kutulia na Nay wa Mitego na
mipango ya uhusiano wao ipoje, alikataa kufunguka moja kwa
moja.“Kiukweli Nay ni mshikaji wangu tu, unajua nini? Kwa sasa siko
tayari tena kumwanika bwana au mchumba wangu kama nilivyofanya mwanzo
kwa Dallas, nitakuja kumweka wazi labda mwanaume nitakayezaa naye au
atakayenioa kabisa,” alisema Wolper.
Kwa upande wake Nay alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Wolper na hatua
ya kuunadi uhusiano wao mtandaoni huku ikifahamika kuwa ana mchumba
mwingine, hakutaka kufafanua zaidi ya kujibu:
“Mimi huwa siangalii nani atasema nini wala atafikiria nini, mimi
nilimmisi Wolper wangu, sikuwa na namna zaidi ya kutumia peji yangu kama
nilivyofanya, tena siku hiyo alikuwa hapatikani hewani nikaamua
kumtupia mtandaoni bila hofu kwani ni mtu wangu wa karibu na siogopi
kitu juu yake,” alisema Nay wa Mitego.
GPL