Wabunge wataka kumchangia Msanii Prof Jay Bungeni, Spika atoa mwongozo

Admin Updates1 year ago4 Views

Wabunge waonyesha nia ya kutaka kumsaidia aliyewahi kuwa Mbunge wa Mikumi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambaye pia ni mwanamuziki wa Hip Hop, Joseph Haule maarufu Profesa Jay.

Hii ni baada ya Profesa Jay kutambulishwa bungeni Dodoma kama mgeni leo Alhamisi Novemba 09, 2023; ambapo hoja hiyo ya kumchangia ilitolewa.

Baada ya hoja hiyo kutolewa, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson alitoa mwongozo kwa kila mtu kuchanga kiasi chochote alicho nacho ambapo mchango huo utakusanywa leo na kisha atakabidhiwa fedha iliyopatikana.

Profesa Jay amekuwa akisumbuliwa na figo kwa takribani mwaka mmoja na miezi mitatu, hata hivyo kwa sasa afya yake inaendelea kuimarika.


 

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.