VANESSA MDEE ‘MIMI HUWA SISOMI MAONI YA MASHABIKI MTANDAONI, WENGI WANAHARIBU HALI YA HEWA KWA MATUSI’

Admin Updates10 years ago5 Views

Mastaa wengi wamekuwa wakitukanwa na kupewa maneno ya hovyo katika
mitandao ya jamii. Mara kadhaa maneno machafu hutolewa baada ya msanii
kuandika lolote au kuweka picha.

Mshindi wa Tuzo ya Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki,Vanessa Mdee
‘Vee Money’ amesema hana utamaduni wa kusoma maoni ya mashabiki wake,
kwani alijaribu kufanya hivyo akaona yanampa msongo wa mawazo.

“Sisomi maoni ya mashabiki kwa sababu walio wengi wanaharibu hali ya
hewa. Mtu utarudi nyuma kwa kuwaza mambo ya watu, ukiona Nick Minaj
ameweka kitu kwenye ukurasa wake haimaanishi kwamba anapenda, ni sehemu
ya kazi,” alisema.

“Nilipotaka kutumia rangi katika video yangu nilikuwa nimepanga na
isitoshe ilikuwa ni wazo jipya. Sipendi kila kazi yangu ifanane na za
wengine, suala la kuwa na vitu vingi linakuongezea, zile rangi
mbalimbali ni wazo la watu.

Walio wengi hawakujua video hiyo wala hawafahamu rangi zilimaanisha nini,” alisema Vee Money.

Qoute of the Day
‘You’ve gotta dance like there’s nobody watching,
Love like you’ll never be hurt,
Sing like there’s nobody listening,
And live like it’s heaven on earth.’

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...